📌BARNABA KISENGI.
MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mh Antony Mavunde ameongozana na wataalamu kutoka wakala wa barabara za mjini na vijijini TARULA kukagua na kuona barabara za mtaa wa chinyoya Kata ya kilimani jinsi miundombinu ya barabara hizo za mtaa wa chinyoya zilivya haribika kutokana na vua zinazoendelea kunyesha na kupelekea kushindwa kuingilika kwa vyombo vya usafiri katika mtaa huo
Awali akitoa taarifa ya kuharibika kwa miundombinu hiyo ya barabara mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo wa chinyoya Bi Faustina Bendera amesema mvua za mwaka Jana na mwaka huu zimeharibu sana miundombinu ya barabara hizo na kuufanya mtaa wake kuwa Kama kisiwa kwa kushindwa kupitika kwa vyombo vya usafiri
"katika kipindi hichi cha mvua za masika kwakweli mtaa wangu umeaadhirika sana safari hii kwa kuaribika kwa miundombinu za barabara za mtaa mzima hazipitiki kwa vyombo vya usafiri kwa sasa zinapita badaboda tu tena kwa shida Sana "Faustina"
Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo ya kilimani Mh Neema Mwaluko amesema Tarura waliangalie jambo hilo kwa mapana maana miundombinu hiyo ya barabara za mtaa wa chinyoya zimeharibika sana na mtaa huo kwa sasa umesha pimwa katika Nyumba za makazi hivyo ni jukumu la tarula kuhakikisha wanazitengeneza barabara hizo
Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Antony Mavunde akiwa na wataalamu hao wa Tarula wamezikagua barabara zote za mtaa huo na kushauriana na wataalamu hao kujua cha kufanya katika kipindi hichi cha mvua kuona wanaweza kuaangalia nini kifanyike wakati yeye Kama mbunge kwa kushirikiana na diwani kuhakikisha katika kipindi hichi cha bajeti ya serikali wanaliwekea umuhimu wa jambo hili la miundombinu za barabara za mtaa huo wa chinyoya ziwekewe bajeti kwakuwa mtaa huo sasa umekwisha kupimwa na wananchi sasa wanamiliki aridhi yao
Wataalamu kutoka Tarula wamesema kwa sasa wanasubiri mvua zipungue ili waweze kuingiza mitambo yao Kama katapila ili waweze kuzichonga barabara hizo za mtaa wa chinyoya kwakuwa kwa sasa katapila halitaweza kuingia kutona na kukwama kwa maji ambayo yamekuwa mengi aridhini ila pindi yakipungua tu watahakikisha wanazitengeneza barabara hizo zote za mtaa huo kwakuwa sasa umekwisha kupimwa na wanahaki ya kutengenezewa miundombinu hiyo
Ziara hiyo ya mbunge ya kukagua miundombiniu hiyo ya barabara iliwashirikiaha diwani wa Kata ya kilimani Neema mwaluko, mwenyekiti wa mtaa wa chinyoya Faustina Bendera,wataalamu kutoka Tarula na viongozi wa chama cha mapinduzi tawi la chinyoya
Mwisho
0 Comments