TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Moshi,01.03.2021
Waziri
wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda (Mb) ametoa tathmini ya kazi ya kuwadhibiti
nzige wa jangwani waliovamia nchi mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu na kuwa
hadi sasa wamedhibitiwa na wataalam wa Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya za Longido, Siha na
Simanjiro.
Prof.
Mkenda ameeleza hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari Moshi mkoani
Kilimanjaro kuwa mapambano dhidi ya nzige yanaendelea vizuri na kuwa hadi sasa
hakuna madhara yoyote kwenye maeneo ya kilimo na mifugo ya wananchi na kuwa jitihada
za kuangamiza makundi yaliyobakia zinaendelea
kwa kutumia helkopita na mabomba ya kupiliza kwa mikono.
“Tupo makini kuwakabili nzige hadi sasa
hatujapata madhara yoyote kwa mashamba ya wakulima hivyo watanzania wasiwe na
taharuki “alisisitiza Prof. Mkenda.
Kuhusu
mikakati ya kupambana na nzige Waziri Mkenda amesema hadi leo tarehe 01 Machi
tayari kuna helkopta kutoka Shirika la Nzige Wekundu (RLCO) na kuwa serikali
itaongeza ndege ya pili kutoka shirika la Nzige wa Jangwani (DLCO) kupulizia
makundi madogo ya nzige walionekana maeneo ya wilaya za Longido kufuatia uwepo
wa taarifa kuwa nzige wachanga kutoka Kaunti ya Machakos nchini Kenya wanaweza
ingia Longido.
Mwisho.
Revocatus Kassimba
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
0 Comments