📌FAUSTINE GIMU GALAFONI
MRATIBU wa Damu Salama jiji la Dodoma Jerome
Malando amesema mahitaji ya Damu salama katika jiji la Dodoma ni chupa hamsini
huku wito ukitolewa kwa kila mmoja kuguswa kuchangia damu salama ili
kuokoa maisha ya watu.
Malando amebainisha hayo leo Machi,20,2020
katika kanisa la Waadventista Wasabato Kikuyu jijini Dodoma wakati wa
uchangiaji wa Damu Salama bure katika kuadhimisha Juma la Matendo ya
Huruma kanisa la Waadventista Ulimwenguni.
Mratibu huyo wa Damu salama katika jiji la
Dodoma amesema damu ina mahitaji makubwa katika uhai wa binadamu na haiwezi
kuzalishwa katika kiwanda chochote hivyo ni muhimu kila mmoja kuguswa
kuchangia damu ambapo jiji la Dodoma lina uhitaji wa chupa 50 za damu kila
wiki.
“Damu ina mahitaji makubwa kwa makundi
mbalimbali mfano akina mama wajawazito,watoto,wazee,watu wanaopata ajali,wenye
selimundu[sicklecell] hivyo ni wito kwa kila mtu kutoa damu kwani ina
umuhimu mkubwa na damu haizalishwi viwandani kama bidhaa zingine na
mahitaji ya damu katika jiji la Dodoma ni chupa 50 kwa wiki”amesema.
Malando ametumia fursa hiyo kulipongeza kanisa
la Waadventista Wasabato kwa kuwa na desturi ya kuadhimisha matendo ya huruma
kwa kutoa misaada mbalimbali kwa jamii ikiwemo kuchangia damu huku
Mzee wa kanisa la Waadventista Wasabato Kikuyu Elias Aron akielezea jinsi
walivyoguswa katika utoaji wa damu salama .
“Kwa kweli nitumie fursa hii kulipongeza
kanisa la Waadventista Wasabato kwa kuwa na huduma muhimu kabisa ya
kijamii ya Juma la matendo ya huruma ambayo inafanyika katika maeneo mbalimbali
nchini ikiwemo utoaji wa damu bure kabisa “amesema.
Kwa upande wao baadhi ya
washriki kwa Kanisa la Waadventista Wasabato Kikuyu akiwemo Samwel
Makumil,Deus Mchoo,Victoria Mkama pamoja na Paula Kazima wamesema suala la
uchangiaji wa Damu ni sehemu ya ibaada katika kuokoa watu wenye matatizo
mbalimbali.
Kanisa la Waadventista Wasabato kote
ulimwenguni huwa linafanya Juma la Matendo ya Huruma kila ifikapo mwezi Machi
ya kila mwaka ambapo huduma mbalimbali hutolewa kwa wahitaji ikiwa ni pamoja na
uchangiaji wa damu bure,kutembelea wafungwa,watoto yatima pamoja na wazee kwa
kuwafariji katika kuwapa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula
,mavazi,sabuni.
0 Comments