KATA YA CHAMWINO YAANZISHA JUMUIYA ZA UFUNDISHWAJI KWA WALIMU.

 


📌Joyce Kasiki.

 KATA ya Chamwino wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma imeandaa Jumuiya ya ujifunzaji kwa shule zilizopo katika kata hiyo.

Lengo la Jumuiya hiyo ni kujengeana uwezo kwa walimu wa madarasa ya awali kujifunza mbinu mbalimbali za ujifunzaji na ufundishaji kwa watoto wa darasa la awali.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii,Afisa Elimu wa Kata hiyo Catherine Chilongani amesema,wameunda Jumuiya hiyo kutokana na mafunzo yaliyotolewa na Shirika linaloangazia katika Malezi na Makuzi ya Maendeleo ya mtoto ya awali (CiC) ili kuhakikisha walimu wote wa madarasa ya awali katika kata hiyo wanaongeza uelewa katika ujifunzaji na ufundishaji wa darasa la awali.

"CiC wanatekeleza mradi wa Watoto Wetu Tunu Yetu katika wilaya ya Chamwino ambapo katika kata  yetu ya Chamwino shule msingi  Kambarage  ipo kwenye mradi huo ,na watu ambao tumepata mafunzo ni wachache,

 " Hivyo sisi tuliopata mafunzo tumeanzisha Jumuiya hii ili kuhakikisha na walimu wengine ambao hawajapata mafunzo wanapata angalau mbinu chache za ufundishaji wa darasa la awali."amesema Chilongani

 Aidha Chilongani amesema,miongoni mwa mambo ambayo wamebadilishana ujuzi ni pamoja na kufanya maboresho ua darasa la Elimu ya awali kwa kulifanya darasa kuwa changamshi na linaloongea tofauti na awali kabla ya kupatiwa mafunzo.

 "Mafunzo haya yametupatia faida nyingi ,maana pia tumeweza kuwaelimisha wazazi juu ya umuhimu wa mtoto wa darasa la awali kupata chakula na mwitikio ni mkubwa kwa wazazi kuchangia chakula." Amesisitiza na kuongeza

"Mbinu za ufundishaji na ujifunzaji zimeboreshwa siyo tu kwa shule za mradi ,hadi shule ambazo hazipo kwenye mradi ,madarasa yote yamesheheni zana kitu ambacho kimeamsha ari ya watoto kusoma na mahudhurio shuleni."

 Vile vile amesema baada ya mafunzo waliona umuhimu wa watoto wa darasa la awali kutengewa chumba kizuri chenye madirisha na mlango unaofunga vizuri kwa ajili ya utunzaji wa zanazinazikuwa darasani.

 "Mfano katika shule ya Kambarage hakukuwa kabisa na darasa kwa ajili ya watoto wa awali,badala yake watoto hao walikuwa wakisomea nje kwenye mlima,lakini baada ya mafunzo tumeona umuhimu na kupitia Juimuiya yetu ya ujifunzaji ambapo walimu wote wa darasa la awali hukutana na kupeana mafunzo na hivyo shule zote tatu katika kata ya Chamwino ,madarasa ya awali hana madarasa tena yanayoongea." Amesema

 Kwa upande wake mwalimu wa darasa la awali kutoka shule ya msingi Chamwino Rhoda Chomola  amesema kutoka na na mafunzo anayopata kutoka wengine waliopata mafunzo kutoka CiC ,amwkuwa na mabadiliko makubwa hali inayomfanya alifurahie darasa licha ya kuwa na wanafunzi wengi.

Amesema mafunzo hayo yamemfanya afahamu Jinsia ya kulifanya darasa liwe changamshi na kivutio kwa watoto na hivyo kuwafanya wapende kujifunza zaidi.

"Mimi nilipoanza kufundisha darasa la awali sikuwa na mafunzo yoyote maana nilichaguliwa tu kufundisha huko baada ya aliyekuwepo kustaafu,lakini baada ya mafunzo haya sasa darasa langu lina zana za kutosha na hivyo kulifanya kuwa darasa linaloongea . " amesema Chomola

Naye mwalimu darasa laawa kati shule a mig Mkapa wilaani Chamwino Joyce Athanas amesema mafunzo hayo yamemsaidia katika utwngenezaji wa zana rahisi zinazopatikana katika mzingira yao ambazo hunsaidia mwanafunzi wavdarasa l awali kujifunza nakuelewa kwa aharaka.

"Mafunzo ninayoyapata kutoka kwa mwenzetu walioshiriki yamenisaidia vitu vingi ikiwemo kutebgeneza zana kwa kutumia chupa za maji,kuchora picha ambazo hulifanya darasa kuwa changamshi.

Hata hivyo mwalimu huyo anasema bado anakabiliwa na changamoto ya wingi wa watoto darasani kutoka na na darasa kuwa dogo.

CiC linatekeleza mradi wa Watoto Wetu Tunu yetu katika wilaya ya Kongwa na Chamwino ambapo pamoja na mambo mengine Shirika hilo linayaboresha mafarasa ya awali katika shule za mradi pamoja na kuweka miundombinu mbalimbali zikiwemo zana za kujifunzia na kufundishia kwa lengo la kumpa mtoto wa darasa hilo msingi mzuri katika ujifunzaji wake.

Post a Comment

0 Comments