📌MWANDISHI WETU.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Consolata Ishebabi amewaasa
watumishi wa Wizara ya Viwanda kutumia mafunzo ya KAIZEN katika kuongeza tija
na ubora katika utendaji kazi na katika majukumu yao ya kila siku.
Consolata ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya
Maendeleo ya Viwanda Vidogo wa Wizara ya Viwanda na Biashara ameyasema hayo Jijini Dodoma katika ufunguzi
mafunzo ya KAIZEN kwa watumishi wa Wizara hiyo yaliyofanyika leo katika Chuo
cha Biashara CBE jijini Dodoma, amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha
watumishi wa wizara kubadili mtazamo, kuongeza tija uwajibikaji na ubora mahala
pa kazi.
Amewasisitiza watumishi hao kutumia S tano ( 5)
ambazo ni Sasambua (Sort), Seti (Seti), Safisha (Shine), Sanifisha
(Standardize) na Shikilia (Sustain)
katika kutekeleza KAIZEN mahala pa kazi na kwenye maisha yao ya kila
siku.
Amesema mafunzo hayo pia yanalenga kuongeza ufahamu
kuhusu mfumo wa falsafa ya uongezaji thamani endelevu wa tija na ubora
viwandani ili waweze kushiriki kikamilifu katika kufanikisha utekelezaji wa
falsafa hiyo katika sekta wanazozihudumia.
Dkt. Ishebabi pia amesema mafunzo hayo yanaongozwa
na kauli mbiu isemayo "KAIZEN kwa Tanzania ya Viwanda Shindani kwa
Maendeleo Shirikishi".
kauli mbiu hiyo inaendana na azma ya Serikali ya
awamu ya tano inayodhamiria nchi yetu kuwa na uchumi wa kati wa Viwanda ifikapo
mwaka 2025.
Mradi wa KAIZEN inayofadhiliwa JICA unalenga
kuongeza tija na ubora katika sekta ya viwanda na shughuli za maisha ya kila
siku inaongozwa na misingi ambayo ipo katika ubunifu wa mawazo, maarifa na
ushiriki wa kila mtu ndani ya taasisi, shirika au kampuni.
KAIZEN ni neno la kijapani lenye maana ya badilika
kwa ubora / uzuri linalohusu shughuli endelevu zinazofanyika ili kuboresha kazi
mifumo michakato na nyanja yoyote ya kuendesha biashara. KAIZEN asili yake ni
Japani lakini sasa inatekelezwa Duniani kote.
MWISHO.
0 Comments