📌FAUSTINE GIMU
WAZIRI wa elimu
Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewaongoza wakazi wa Jiji la
Dodoma kuuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu kiongozi, John Kijazi kwenye
hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH)
Akimzungumzia
Marehemu Kijazi, Profesa Ndalichako alisema alikuwa ni mtu mpole,
mnyenyekevu,mtulivu mchapakazi na mzalendo aliyekuwaanafanya kazi yake
kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake
Katibu Mkuu Ikulu, Moses Kusiluka amesema ibada ya kiserikali ya kumuaga
Marehemu Balozi Kijazi itafanyika kesho Jijini Dar es Salaam
kwenye ukumbi wa Karimjee ambapo Rais John Magufuli atawaongoza wakazi wa
Dar Es Salaam kuuaga mwili huo kabla ya kusafirishwa kwenda
nyumbani kwao Wilayani Korogwe mkoani Tanga kwa mazishi yatakayofanyika
kesho kutwa.
Naye Makamu mkuu
wa Chuo Kikuu cha Dodoma, (UDOM) Profesa Faustine Bee amesema alikuwa anatamani
kuendelea kufanya kazi na Balozi Kijazi kwani hata katika changamoto nyingi za
chuo hicho walikuwa pamoja katika mapambano ambapo haki ,wajibu na
unatawala vilidumu katika kupelekea watanzania kukimbilia
chuo kikuu cha Dodoma kusoma na kufanya kazi.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma
Dkt.Binilith Mahenge amesema Marehemu Balozi Kijazi katika kipindi cha uhai
wake alikuwa mstari wa mbele katika harakati ya serikali kuhamia Dodoma huku
Mkurugenzi wa hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa Dkt.Alphonce Chandika
akizungumzia utii wake wakati akipata matibabu hospitalini hapo.
Balozi Kijazi
aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali hiyo Jijini
Dodoma alipokuwa amelazwa kwa matibabu anatarajia kuzikwa siku ya Jumamosi,nyumbani kwao Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga.
Balozi John Kijazi Agost,2020 aliteuliwa kuwa mkuu wa Chuo
Kikuu cha Dodoma kutokana na aliyekuwa Mkuu wa Chuo hicho Benjamin
William Mkapa kufariki Dunia.
0 Comments