📌STEPHEN NOEL.WATALAAM wa afya
wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wasambaa katika tasisi za serikali
ikiwamo shule za Msingi, sekondari, kwenye Nyumba za wageni kutoa elimu dhidi ya magonjwa ya mlipuko kama
kipindu pindu, magonjwa ya matumbo pamoja na ugonjwa Corona au COVID -19.
Jopo hilo likiongozwa
na mganga mkuu wa wilaya hiyo Dkt Archard Rwezahura amesema wizara Afya
maendeleo ya jamii jinsia,wazee na watoto ina utaratibu wa uelimishaji jamii
juu hatua za kuchukua dhidi ya magojwa ya mlipuko yanapo tokea na
wananchi kuchukua tahadhari juu ya magonjwa hayo.
Amesema lazima
wananchi wa wilaya hiyo kuchukua tahadhari ili kujilinda wao wenyewe na
familia zao kwa jaguars kanuni za Afya.
Naye afisa Afya wa
wilaya Mery Mabagwa amesema wameamua kutoa elimu ikiwa na lengo ni
kuwakumbusha jamii juu ya kanuni za afya kujikinga na magonjwa ya mlipuko ya
aina zote ikiwamo korona.
Amedai Kama wilaya
tayari wameshajipanga kutoa elimu kwa tasisi zote zikiwamo shule vyuo, tasisi
za dini na nyumba za wageni, na kuiomba jamii kuendelea kuchukua tahadhari na kufuata maelekezo ya wizara ya afya.
Mmoja wa wazee wa jadi
wilayani Hapa bwana Hassan Kiwogosa amesema pamoja na watalaam kutoa elimu hiyo
ya tahadhari pia serikali iboreshe huduma za jamii ikiwamo upatikanaji wa
uhakika wa maji katika mji wa Mpwapwa na upatikanaji wa dawa katika hospitalini
na katika vituo vya afya huko vijijini .
Hata hivyo
amesema jamii ipende kutumia dawa za asili ikiwamo kujifukiza na
dawa zingine ambazo zilitumiwa na wahenga kipindi chao na zikawasaidia.
Naye Magreth
Boma Mhudumu Hotelin ameiomba serikali na kusema pamoja na kupewa elimu
njisi ya kujikinga na kununua dawa hizo lakini serikali iweke mkakati wa vipimo
Kwa wageni wanao ingia ndani ya wilaya.
Mwisho.
0 Comments