📌JASMIN SHEMWEPU.
Serikali imewataka wananchi kujiunga na mfuko wa Afya ya jamii CHF iliyoboresha kwani imekuwa msaada mkubwa kule inakotumika kwa kuwa inarahisisha matibabu kwa jamii ikiwemo kupata Dawa kwa wakati mtu anapopata matatizo ya kiafya .
Aidha wakuu wote wa mikoa nchini wametakiwa kuwa wahamasishaji wakubwa kwa wananchi kujiunga na CHF iliyoboresha kwani inasaidia kupunguza gharama za afya kwa kusogeza huduma bora ikiwemo dawa na vitendanishi kwenye maeneo yote ya kata,vijiji,mitaa na vitongoji.
Naibu waziri ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia afya Dr.Festo Dugange amesema hayo katika hafla ya kukabidhi kadi za CHF iliyoboreshwa ICHF kwa wananchi wa makundi mbalimbali ikiwemo makundi maalum kutoka kaya 361,539, kadi zenye thamani ya shilingi bilioni 4.6 chini ya wadau HPSS na shirika la PACT .
Akizungumza katika hafla hiyo mkurugenzi wa huduma za afya ofisi ya Rais TAMISEMI Dr.Ntuli Kapologwe pamoja na kuwapongeza wadau wa maendeleo HPSS na PACT kwa mchango mkubwa katika sekta ya afya kwani lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025 Bima ya afya inakuwa ni kwa wananchi wote na kuondokana na utegemezi pamoja na kuwa na vyanzo muhimu vya mapato kuendesha shughuli za afya.
Naye Meneja mradi wa HPSS Tuimarishe Afya Ally Kebby ameelezea kufurahishwa kwake na namna CHF iliyoboreshwa inavyozidi kupokelewa na wananchi katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba wataendelea kuunga mkono jitihada za serikali kwa kuzidi kutoa elimu kwa wananchi wa makundi yote.
Upande wake mmoja wa wanufaika wa mradi huo wa HPSS Tuimarishe Afya maarufu mradi wa Kizazi kipya Julie Ezekiel kutoka Hombolo Makulu, ameshukuru kwa kupata kadi ya CHF iliyoboreshwa na kuwataka wananchi wengine kujiunga na mfuko huo.
0 Comments