Wakizungumza
na waandishi wa habari leo(25.02.2021) baadhi ya wakulima walimweleza Naibu Waziri wa Kilimo Hussein
Bashe aliyetembela mashamba ya Nanai eneo la Sanya Juu wilaya ya Siha
kufuatilia kazi ya kuangamiza nzige ikiwa ni leno la serikali kulinda maisha ya watu na
mali zao.
Mzee
Felix Mosha mkulima na mmiliki wa shamba la Kafori West Kilimanjaro alisema
tukio la kuvamiwa na nzige juzi lilileta taharuki kwa wakazi wa maeneo hayo kwa
kuwa sasa ndio wameanza kupanda mazao mashambani lakini wamefarijika kuona
hatua za serikali chini ya wizara ya Kilimo kuwadhibiti nzige
hao.
“Tunaishukuru
serikali kwa kuja kwa haraka, leo tumeona wataalam wamefanikiwa kuwaangamiza
nzige waliovamia mashamba yetu ya makademia na ngano yanaendelea kuwa salama” alisema Mzee Mosha.
Akizungumzia
operesheni kuangamiza nzige, Naibu Waziri Kilimo Hussein Bashe alisema mpaka
sasa hali ya kuangamiza nzige tangu walipovamia maeneo ya Tanzania inaendelea
vizuri na wadudu wamedhibitiwa kwa kupuliziwa viuatilifu kuwaua kwa njia ya ndege na mabomba ya kushikwa kwa
mikono.
Bashe
alisema kuwa wizara inatambua wilaya ya
Siha ni muhimu kwa kilimo hivyo lazima itazamwe kwa karibu nzige wasije haribu ndio
maana wanaendelea kwenda kujionea kazi ya kuwadhibiti nzige hao ambapo
ameshuhudia makundi ya nzige waliokufa baada ya kupuliziwa sumu.
Bashe
aliongeza kusema wizara imeongeza vifaa vya kusaidia kupambana na nzige pia imeanzisha
mafunzo kwa maafisa ugani wa vijiji na kata kutambua aina za nzige ili iwe
rahisi kudhibiti pale watakapojitokeza kwenye maeneo yao
“Mpaka
sasa Longido tumefanikiwa kwa asilimia 95 zoezi limefanikiwa hakina masalia ya
nzige ambapo nzige waliovamia Siha walitokea Longido baada ya kundi lao
kupuliziwa sumu hivyo wakakimbia na sasa
tumewafuata hapa Sanya Juu tumewaua? Alisema Bashe.
Bashe
aliongeza kusema kazi ya kudhibiti nzige wilaya ya Simanjiro imeenda vizuri
ambapo hadi sasa taarifa za wataalam zinaonesha kumebakia kundi moja
lililolojificha kwenye milima na kazi ya kulifuatilia ili liangamizwe.
“Hadi
sasa hakuna madhara yoyote kwenye mazo ya wakulima tanagu nzige wavamie nchi
hapa mwezi Janauri mwanzoni. Ni heri tupate madhara ya kufa kuku lakini nzige
lazima tuwatafute kokote waliko “
alisisitiza Waziri Mkenda
Kwa
upande wake Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia za visumbufu Taasisi ya Udhibiti wa
Viautilifu kwenye Ukanda ywa Kitropiki (TPRI) Mhandisi Julius Mkenda alieleza
kuwa kundi la nzige lililovamia wilaya ya Siha ni baadhi ya waliokimbia Longido
baada ya kazi ya kunyunyizia kiuatilifu tarehe 22 mwezi huu hivyo wakatoroka na
kuingia Siha na kuwa siyo kundi jipya kwa mujibu wa utafiti waliofanya.
Mhandisi
Mkenda alibainisha kuwa nzige waliovamia Siha wanaendelea kuangamizwa kwa
kutumia ndege maalum pia mabomba ya kupuliza kwa miko kwa wale walio jirani na
makazi ya watu ambapo zoezi limeenda
vema jana na leo na kuwa wataendelea kuchukua hatua za kuwadhibiti .
“Jambo
kubwa kwa Siha ni kuwa nzige hawa wana
siku tatu tayari wameanza kuwa wa njano toka wekundu hali amabyo ni hatari hivyo sasa tunawafundisha maafisa
ugani wa kata na vijiji wajue namna ya kuwatambua na kuwadhibitipindi
wakijitokeza tena” alisisitiz Mhandisi Mkenda.
Waziri
wa Kilimo pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo wapo kwenye mikoa ya Arusha na
Kilimanjaro kufanya ufuatiliaji wa karibu wa udhibiti wa makundi ya nzige ili
wasije haribu mashamba ya wakulima.
Mwisho
Imeandaliwa
na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo
SIHA
26.02.2021
0 Comments