📌RAMADHAN
HASSAN.
WAKAZI
wa Kata ya Wisikwantis Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma wanalazimika kunywa
maji ya kwenye madimbwi kutokana na kutopata maji safi na salama tangu
kupatikana kwa uhuru.
Pia
wamesema licha ya kuwa Mjini lakini hakuna barabara za kuweza kufika
katika eneo hilo pamoja na kukosekana kwa huduma ya umeme hali ambayo
imekuwa ikiwapa wakati mgumu.
Wakizungumza
na Waandishi wa Habari leo Februari 2 mwaka huu,Wakazi hao wamedai kwamba
maisha kwao yamezidi kuwa magumu kutokana na kutopata huduma za kijamii kwa
muda mrefu.
Mohammed
Soloka amesema kwamba licha ya kwamba wapo mjini lakini kwao huduma ya maji ya
bomba imekuwa mtihani mkubwa kwani tangu upatikane uhuru hawajawahi
kuipata.
Soloka
amesema licha ya kupiga kelele na kupaza sauti hakuna ambeye amekuwa
akiwasaidia huku wakazi wa eneo hilo wakichimba mashimo katika makorongo zaidi
ya mita mbili ili kupata maji.
“Wakati
wa masika huwa afadhali kwani huwa tunachimba vishimo vidogo tunatoa yale maji
machafu tunachota masafi,kiangazi ni mchanga tu hili korongo
linatoka katika maeneo ya Bolisa na Ghubali lakini wakati wa
kiangazi ni shida tupu tunachimba mpaka mita mbili ndio tunapata
maji,”amesema Soloka.
Kutokana
na hali hiyo wameiomba Serikali iwasaidie ili waweze kupata maji ya bomba
kwani wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu.
Pia,
Soloka amesema licha ya maeneo ya jirani kuwa na umeme lakini wao wamekuwa
wakiishi gizani ambapo amedai ni kama wametelekezwa huku wenye Mamlaka wakiwa
kimya.
“Mbunge
wetu hata upige simu vipi hapokei.Tunaishi maisha ya shida sana,hapa hatuna
umeme wanaohusika kila siku wanatupa majibu rahisi tu sasa tunaiomba Serikali
itusaidie,”amesema Soloka.
Vilevile,amesema
wanakabiliwa na changamoto ya barabara kuwa mbovu katika eneo hilo hali ambayo
imekuwa ikiwapa wakati mgumu.
“Huku
kwetu ni makorongo mtindo mmoja,shida inakuja mama mjamzito akitaka kupelekwa
Hospitali haiwezekani kwani gari haiwezi kufika,magari hayafiki huku kwetu
hakuna barabara,”amesema Soloka.
Alipotafutwa
kwa njia ya simu Mwenyekiti wa Kata hiyo,Mwahu Ibuma alisema kwamba yupo
kwenye kikao na alipotafutwa kwa mara nyingine alidai yupo safarini.
Kwa
upande wake Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mjini,Ally Makoa (CCM) alipotafutwa kwa
njia ya simu,simu yake iliita bila kupokelewa kwa zaidi ya mara 5.
0 Comments