📌HAMIDA
RAMADHANI.
SHIRIKISHO la Vyama
vya Wafanyakazi Nchini TUCTA,limeiomba Serikali kuwaongeza mshahara Wafanyakazi
katika sekta zote nchini zikiwemo Sekta binafsi katika bajeti ya Mwaka huu kwa
lengo la kuwaboreshea maslahi watumishi.
Kauli hiyo imetolewa
Jijini Dodoma na Rais wa Shirikisho hilo,Tumaini Nyamuhoka wakati
akifunga Kikao kazi kwa Makatibu wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa
(TALGWU)yaliliyolenga kuwajengea uwezo.
Nyamuhoka amesema
wanampongeza Rais kwa jitihada mbalimbali ambazo amekuwa akizifanya katika
kuleta maendeleo huku wakimuomba kuliangalia suala hilo kwa kina la
nyongeza ya mshara yema Sasa
"Tunampongeza
Rais Magufuli kwakuwarudisha kazini watumishi ambao wana Elimu ya darasa la
Saba huku akiomba kuwalipa mishara yao kwa kipindi ambacho walikuwa hawapo
kazini," amesema Nyamuhoka.
Ametoa wito kwa
Wakurugenzi Halmashauri,Wakuu wa Taasisi pamoja na Makatibu Tawala Nchini
kuacha kuwadharau Viongozi wa Wafanyakazi na badala yake wawape kipaumbele
kwa kuwasikiliza .
Hata hivyo amekemea
suala la baadhi ya Maofisa kuwekwa ndani kutokana na kuwapa Fedha Viongozi wao
licha ya wao kutokuwa na makosa kutokana na kuagizwa tu kufanya hivyo.
Kwa upande wake Mweka
Hazina wa Talgwu Taifa Siston Mizengo ameeleza mafanikio
yaliyopatikana kutokana na kuweza kutekeleza mipango yake iliyojiwekea na
kwasasa kipo vizuri na ilipata hati Safi
0 Comments