📌STEPHEN NOEL.
TASISI za Masada
kisheria na za kutetea Haki na zinazo toa msaada wa kisheria zimeobwa kufungua
ofisini zao vijiji tofauti na sasa ambapo tasisi nyingi zimejikita mjini
na makao makuu ya wilaya.
Ombi hilo limetolewa
na wanachuo wa chuo cha walimu Mpwapwa katika kuelekea kilele cha wiki la
sheria na miaka 100 ya kuanzishwa kwa mahakama kuu walipo kuwa wakiongea
chama cha majaji na mahakimu wanawake TAWJA( Tanzania Women Judges
Association).waliofika chuoni hapo kutoa Elimu.
Bwana Athuman Lan'gu
mwanachuo mwaka wa tatu amesema kuwa vyama vingi vinavyotoa misaada ya kisheria
wamejikita kufungua ofisi mijini na makao makuu ya wilaya ambapo changamoto
nyingi zinakuwa vijiji kutokana na uelewa mdogo wa masuala mtambuka ya maisha
haki na maendeleo yao.
Amedai kuwa
changamoto nyingi zinazo wakabili watu wa vijijini ni ukatili wa kijinsia,
migogoro ya Ardhi ,ndoa na masuala ya kuhusiana na wosia na miradhi ambayo watu
wengi hupoteza haki zao kutokana na kushidwa kuelewa changamoto zao
zinatatuliwaje.
Naye Eisante Nassaly
amesema kuwa pamoja na changamoto hizo pia jamii za vijijini zinakabiliwa
na changamoto nyingi za masuala ya haki ambayo Tasisi za utetezi ziweze
kuwasaidia bila kujali mazingira waliopo.
"Najua inaweza
ikawa ngumu kulingana na mtaji lakini bora wangekuwa wanatoa huduma za mkoba za
kutembelea vijiji walau Mala moja kwa miezi mitatu ili kuweza kuwasaidia watu
wa vijijini "aliongea.
Kwa upande hakimu
mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Nurupedesia Nassary alikili kuwapo kwa
tasisi chache za misaada ya kisheria vijijini kunakupelekea kuongezeka kwa
vitendo vya ukatili wa kinjisia na vifo vitokanavyo na wivu wa mapenzi.
Amesema pamoja na
kutokuwapo kwa tasisi hizo wananchi wajenge moyo wakutembelea Mahakama na
kujifunza au kuuliza masuala yanayo watatiza.
Katika kipindi hicho
zaidi ya wanachuo 800 walufundishwa maada za ukatili wa kinjisia, Sheria ya
Wosia na miradhi pamoja , sheria ya ndoa ,na mfumo wa mahakama.
Pia amedai wananchi
waache kuziogopa mahakama wazitumie kujielimisha sheria ndogo ndogo zinazogusa
maisha yao ya kila siku.
Mwisho.
0 Comments