📌DEVOTHA SONGORWA.
MAHAKAMA,ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EACJ) imezitaka Nchi wanachama wa mahakama hiyo kutoa michango
yao ipasavyo ili kuondoa changamoto zinazowakabili mawakili na wanananchi na
kusababisha mlundikano wa kesi.
Hayo yalisemwa leo na Mrajisi Mkuu
wawa mahakama hiyo Yufnalis Okubo katika mazungumzo maalumu na gazeti
hilibambapo alisema ukosefu wa fedha za kuendesha shughuli za mahakama umekuwa
ukidhoofisha utendaji kazi.
"Mahakama bado haijulikani
inafanya nini wanachanganya na ile ya AU kwa sababu wote tupo Arusha na
tunakwama kwa sababu hatuna fedha ya kuzunguka Nchi zote sita za Jumuia kutoa
elimu wakati mwingine wanachama wanasema hawana hela ifike wakati nchi hizi
zione umuhimu wa mahakama kufanya kazi katika hali ya ubora,"alisema
Mrajisi huyo.
Pia Amesema bado wananchi hawana
elimu kuhusu uwepo wa mahakama hiyo na majukumu yake akisema kwamba ilianzishwa
kwa lengo kuwasaidia kupata haki na ufumbuzi wa malalamiko yako pindi Serikali
husika inapokiuka Sheria zake.
"Court hii iliteuliwa kwa ajili
yao japo baadhi wanashindwa kuzitofautisha kazi zetu na mahakama nyingine na
siyo kila kesi inaletwa hapa ila ni zile zinazohusu Serikali kukiuka Katiba ya
Jumuia ya Afrika Mashariki au Serikali kuvunja Sheria yake yenyewe na kuumiza
wananchi, kampuni inayofanya Biashara miongoni mwa Nchi za Jumuia hii anaweza
kufungua kesi dhidi ya Serikali husika endapo haikutendewa haki au mtu yeyote
anaweza kuifungulia mashtaka,"alisema Mrajisi huyo.
Okubo akizungumzia mikakati ya
mwaka 2021 alisema wanatarajia kumaliza kesi nyingi zilizosalia na kuhakikisha
Majaji wote wa mahakama wanaishi mkoani Arusha kwani hulazimika
kuhudhuria mahakamani Mara moja kwa mwezi kutokana na kutokuwa na makazi
maalumu hapa nchini hivyo kusababishwa kuchelewa kusikiliza kesi kwa wakati.
"Tunatarajia Serikali zetu
zitaona umuhimu wa Majaji wetu kuishi hapa nchini kuboresha utendaji kwa mwaka
2020 tumeamua kesi 50 ambazo hazijasikilizwa ni zaidi ya 100 na kila wiki
tunapata kesi mpya kutoka popote ndani ya Nchi wanachama wanachi waitumie mahakama
hii ni yak wasiogope,"alieleza Okubo.
Aidha alieleza kwamba wamekuwa
wakishirikiana na mawakili wa hapa nchini kuwapa elimu ya majukumu yao
kwa kuwapa mafunzo namna ya kuwasaidia wananchi kufanya maamuzi sahihi
kulingana na kesi zao ili kuoata haki.
"Kama mawakili hawaelewi ni
ngumu mwananchi kuelewa Sasa tunashirikina na Kitengo Cha Tanganyika Law
Society (TLS)
ili walete mawakili wao tuwafunze
namna ya kuwaelekeza wnanachi kuchambua kesi ipi isikilizwe na mahakama yetu au
nyingine maana watu wanachanganya unakuta mtu anauliza mambo yanayosimamia na
court ya AU au kuuliza kule masuala tunayofanya sisi,"alieleza Okubo.
Ikumbukwe kuwa Mahakama ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki, iliundwa mwaka 2006 ambapo jukumu kubwa la mahakama
hiyo ya haki ya EAC ni kuhakikisha mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
unafuatiliwa na kulinda utengamano katika ukanda huo ikunganishwa na Nchi sita
za Burundi,Kenya,Rwanda,Sudani Kusini, Tanzania na Uganda.
0 Comments