MBUNGE wa
Nyasa(CCM), Mhandisi Stella Manyanya, amesema sababu za Chama cha
Mapinduzi(CCM), kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu 2020 ni kutokana na
mambo yaliyofanywa na serikali chini ya Rais Dk.John Magufuli.
Akichangia
Mpango wa tatu wa Maendeleo wa Miaka mitano bungeni leo, Manyanya amesema
wananchi wameelewa namna ambavyo CCM imetekeleza yale yaliyoahidiwa na masikio
yao kwasasa wasikiliza mpango huo utawasaidiaje.
“Mpango
huu utakuwa na maana zaidi pale tutakapohakikisha unakuwa na manufaa kwa
watanzania,”amesema.
Aidha,
ameishauri serikali kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa bwawa la uzalishaji
umeme la Mwalimu Nyerere na ujenzi wa reli ya kisasa katika Mpango huo kwa kuwa
miradi hiyo ni mkombozi kwa watanzania.
“Inahitaji
mtu ambaye hakuwepo kwenye mgao wa umeme ashangae Bwawa la Nyerere, ni mtu
atakayeshindwa kujua tunapoteza mapato kutokana na usafirishaji mizigo kutoa
bandarini kupeleka nchi jirani, wana CCM tuna wajibu wa kuelimisha wananchi ili
kujua umuhimu wa miradi hii mikubwa,tuendelee kuisemea hadi
itakapokamilika,”amesema.
Ameomba
serikali kukamilisha miradi hiyo ili isaide upatikanaji wa fedha nyingi za
kuhudumia maeneo mbalimbali katika nchi.
“Tuwe na
fedha kidogo au zaidi lazima miradi hii ya kimkakati ikamilike, pia tuimalishe
ulinzi wa mipaka yetu,”amesema.
Aidha,
amesema maendeleo yanakwenda kwa kasi Nyasa na Mbinga kutokana ujenzi wa
barabara uliofanywa.
“Niombe
yale yaliyoainishwa kwenye Ilani ya uchaguzi ya CCM barabara ya
Chiwindi-Mbambay hadi Litui-Amani makoro na daraja la mitomoni kipande kile
kinadai katika mpango huu mambo yatekelezwe kama yalivyoahidiwa,”amesema.
0 Comments