📌FAUSTINE GIMU.
Katibu mkuu Wizara ya
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Zainabu Chaula amesema juhudi za
pamoja zinahitajika kutengeneza , mazingira ya kukuza matumizi bora
ya mawasiliano nchini.
Dkt.Chaula amesema hayo
jijini Dodoma katika Kikao cha kujadili Mkakati wa TEHAMA
kwenye ngazi ya jamii ikiwemo vituo vya Afya na shule
hapa nchini ,Tanzania Community Digitization[TCD]kilichokutanisha
wadau mbalimbali wa Mawasiliano.
“Juhudi hizi za
pamoja zitatusaidia katika kukuza sekta ya mawasiliano zikiwemo ni pamoja na
mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hii ni katika kuhakikisha mawasiliano
yanafika katika ngazi zote hadi vijijini”amesema.
Aidha,Dkt.Chaula
amesema moja ya malengo ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ni
kuhakikisha taasisi zote za umma zinapata huduma ya Mawasiliano kwa gharama
nafuu ifikapo mwaka 2025 wizara itajipima angalau kufikia asilimia 40% .
Hata hivyo,Dkt.Chaula
amebainisha kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga ni kwa namna gani
inahakikisha inafikisha huduma ya mawasiliano katika maeneo mbalimbali
ambapo wizara imetoa mwelekeo katika kusambaza huduma ya mawasiliano.
“Ndio maana serikali
ina sera ya TEHAMA ya mwaka 2000 na mwaka 2016 serikali ilipitia sera ili
kwendana na mazingira na maendeleo ya Teknolojia ,lazima tutengeneze
mazingira ya Evaluation mwezi uliopita umefanya nini na sasa unafanya nini,na tunatambua
mchango wa sekta binafsi katika mawasiliano hivyo tumejipanga katika
kuhakikisha sekta ya mawasiliano inasonga mbele”amesema.
Pia ,Dtk.Chaula
amesema vyombo vya Habari vina mchango mkubwa katika kuhabarisha umma juu ya
umuhimu wa mawasiliano katika kukuza uchumi wa nchi.
“Kwa nanma moja ama
nyingine wote tunahusika na jambo hili ,tumejenga mifumo mikubwa TAMISEMI
,kupitia level za halmashauri mpaka level za vijiji ,ili mifumo ifanye kazi
vizuri lazima internet connection”amesema.
Mulembwa
Munaku Mkurugenzi wa TEHAMA Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari.
Mkurugenzi wa TEHAMA
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mulembwa Munaku amesema
pamekuwepo na changamoto ya wadau wengi kupeleka huduma ya mawasiliano katika
sehemu moja na wengine kukosa huduma hiyo .
Dkt.Florence Rashidi mkuu wa idara ya mawasiliano ya uhandisi na elektroniki kutoka chuo kikuu cha Dodoma.
Mkurugenzi mtendaji wa
Taasisi ya kutoa majukwaa ya mtandao wa kujifunzia kwa wanafunzi wa
shule za msingi na sekondari[Shule Direct] Faraja Nyarandu amesema
mradi huo umekuja kwa muda muafaka katika kukuza sekta ya mawasiliano nyanja za
elimu huku mkuu wa idara ya mawasiliano ya uhandisi na elektroniki
kutoka chuo kikuu cha Dodoma Dkt.Florence Rashidi akibainisha wamejipanga
kushirikiana
0 Comments