📌FAUSTINE
GIMU
IDARA
ya vijana kanisa la Waadventista Wasabato kanda ya Dodoma imeanza kusajili
vikosi kazi vya vijana ndani ya kanisa kwa mwaka 2021 kwa ajili ya kazi
za utume.
Akizungumza
na mtandao huu alipotembelea kanisa la Waadventista Wasabato
Chang’ombe jijini Dodoma mratibu kiongozi idara ya huduma ya vijana
kanisa la Waadventista Wasabato kanda ya Dodoma Mwinjilisti Mark
Imori alisema lengo la kufanya ziara katika makanisa mbalimbali ni
kuhakikisha wanasajili vijana katika vikosi mbalimbali kwa lengo
kufanikisha kazi za utume pamoja na kutambulisha viongozi wa vikosi vya vijana.
Tupo
mwanzo wa mwaka ambapo makanisa yote yapo katika usajili wa vijana hivyo na
sisi kanda ya Dodoma tumeanza zoezi hili ikiwa ni pamoja na kutambulisha
viongozi wa vijana
Mwinjilisti Imori.
Kwa
upande wake mratibu idara ya vijana kanisa la Waadventista Wasabato mtaa wa
Kizota Dodoma Edwin Tongora alizungumzia sifa za kiongozi wa kikosi
kazi cha vijana kanisani ni pamoja na mwenye juhudi na kusimamia mipango na
kuhakikisha vijana wanaeneza utume.
Adam
Rugazama ni miongoni mwa vijana kutoka kanisa la Waadventista Wasabato
Chang'ombe jijini Dodoma ambapo alisema ni wajibu kwa kila kijana kujitoa
katika kufanya kazi ya utume.
Pamoja
na kusajili vijana,idara ya vijana kanisa la Waadventista Wasabato kanda ya
Dodoma pia imeendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa vijana ikiwemo masomo
ya ujasiriamali ,uchumba na ndoa ,kaya na familia huku ikitambulisha viongozi
wasimamizi wa vijana [Master Guard] kwa mwaka 2021.
Wakati huohuo,Wazazi na Walezi ndani ya kanisa la Waadventista Wasabato wameaswa kuendelea kutimiza wajibu wa kuwafundisha na kuwaelekeza vijana namna nzuri ya Kuendeleza kazi za utume.
Wito huo ulitolewa na mratibu wa vijana kanisa la Waadventista Wasabato
mtaa wa Kikuyu jijini Dodoma mwinjilisti Demetrius Mapesi katika uzinduzi
wa huduma ya vijana Kanisa la Waadventista Wasabato Ntyuka mtaa a
Kikuyu ambapo alisema ni muhimu kuwajengea msingi mzuri vijana katika ukuaji wa
kanisa.
Tutakuwa na kanisa lenye ustawi mkubwa
endapo endapo vijana watafundishwa miongozo mizuri ya
kulitumikia kanisa tuwatie moyo
Aidha,Mwinjilisti Mapesi ametumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwa wa mfano kwa
kufanya matendo mema ndani na nje ya kanisa ili kuondokana na dhana ya
kudharauliwa.
“Ili ujana wako uheshimiwe lazima
ujichunge, uwe na heshima ,upendo ,waefeso 6:4 “alisema.
Hata hivyo alitumia fursa hiyo
kuzungumzia changamoto zinazowakabili vijana ikiwa ni pamoja na
kutosikilizwa,kutopewa nafasi,majibu mabaya, pamoja na kuwa na matabaka
hivyo si vyema kudharau vijana ,Timotheo 1:10.
Kwa upande wake Mzee wa Kanisa la Waadventista Wasabato Ntyuka Stephen Chacha
alisema matarajio ya kanisa ni kuwalea vijana katika misingi bora ya kumtumikia
Mungu.
Nao baadhi ya vijana waliohudhuria katika Sabato hiyo ya vijana akiwemo Yohana
Asheri,Belenice Jackson na Japhet Paul walisema vijana ni nguzo muhimu kwa
maendeleo ya kanisa huku wakiwasihi vijana wengine kujiunga kwenye idara
ya vijana katika kufanya kazi za utume.
Idara ya vijana imeundwa na vyama vitano
vilivyochini ya kanisa la Waadventista Wasabato wakiwemo wavumbuzi miaka
4 hadi 9,watafuta njia miaka 10 hadi 15, mabalozi ,wanafunzi vyuoni
pamoja na vijana wakubwa.
0 Comments