📌BARNABA KISENGI.
MKUU wa wilaya ya bahi mkoani Dodoma Bi. Mwanahamis Mkunda amemwagiza afisa elimu secondary kuhakikisha wanaweka mbinu mpya ya kuandikishana mikataba kati ya idara ya elimu secondary na wazazi na wanafunzi wa kike ambao wanaishi kwenye kaya masikini ambao wanasomeshwa na fedha ya serikali kupita mfuko wa Tasaf unaohudumia kaya masikini wilayani hapo.
Kauli hiyo ameitoa wakati akifunga mafuzo ya siku tano ya watoto wa kike mia moja na tano kutoka shule 17 za wilayani bahi ambapo mafunzo hayo yalilenga kuwapatia elimu ya kujitambua Kama watoto na kujikinga na VVU ukimwi pidi wawepo mashuleni ambapo mafunzo hayo yaliandaliwa na kuratibiwa na ofisi ya waziri mkuu yaliyofanyika jijini Dodoma katika shule ya secondary ya Dodoma kwa siku tano
Hapa nimwagize afisa elimu secondary kuhakikisha sasa anakuja na mbinu mpya ya kuandikishana mkataba na nyinyi wanafunzi na wazazi wenu kuwa mtasoma hadi kumaliza kidatu cha nne bila kupata mimba shuleni hapa tutakuwa tumewanusuru watoto hawa na kwa kuanzia tukaanze na hawa 105 ambao wamepata mafunzo.amesema Bi Mkunda
"Wilaya ya bahi inawafugaji wengi na wananchi kwa kuhamahama pia wazazi wengi wanamaisha duni na hawataki watoto wao wasome hivyo tumefanya kazi kubwa kuwaelimisha watambue umuhimu wa elimu”ameongeza.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi Naibu katibu mkuu ofisini ya waziri mkuu Bi Doroth Mwaluko amesema mafunzo hayo ya siku tano yamewajengea uwezo mkubwa watoto hao wa kike kwa kupatiwa elimu ya kujitambu na kuepukana na VVU ukimwi pindi wawepo mashuleni na kwakuwa mradi huo ulizunduliwa wilayani bahi hiyo watoto hao waonyeshe mfano na mabadiliko chanya kwa jamii huko waliko
"Nitashangaa Sana kwenu mabinti mliopata mafunzo haya kuja kusikia kati yenu moja wenu ameacha shule kwa sababu amepata mimba akiwa shuleni wakati tumewapatia mafunzo hapa utakuwa umetia aibu kwako binafsi na familia yako na wilaya ya bahi kwa ujumla "amesema Mwaluko
Kwa upande wao watoto hao kutoka
wilaya ya bahi waliishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwaletea elimu bila
malipo na wameahidi mafunzo hayo waliyopata ni elimu tosha ya kujikinga na
vishawishi vyote ambavyo watakutana navyo.
0 Comments