📌HAMIDA
RAMADHANI
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa
amezindua kitabu kinachoelezea hitoria ya uongozi wa Rais Dkt. John
Magufuli kipindi cha miaka mitano iliyopita ya uongozi wake.
Aidha
Kitabu hicho kijulikanacho kwa jina la mwanamabadiliko tangu siku ya kwanza
Ofisini (The game Changer presdent Magufuli’s First term in Ofice kimeelezea
kazi za nzuri za maendeleo zilizofanywa na Serikali ya awamu ya Tano katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Waziri Mkuu alizindua kitabu
hicho kilichoandikwa na wahadhiri Wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)wakiongozwa na
Prof. Ted Mallyamkono leo Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbali
mbali wa Serikalini.
Katika kitabu hicho mijadala
mbalimbali imeibuliwa kutoka uongozi mahiri wa Rais Magufuli ambapo majibu
yaliyopatikana huyu ndio Rais aliyeleta mabadiliko
ambaye Wananchi wa Taifa hili walikuwa wakiyatamani kwa miaka mingi.
Amewapongeza wananzuoni hao kwa kuona kazi nzuri iliyofanywa na Serikali ya awamu ya Tano chini ya Dkt. Magufuli na kuamua kuweka katika kitabu ambacho kitasomwa na kizazi hadi kizazi hongereni sana
Waziri Mkuu Majaliwa
Aidha amesema hayo yanayofanywa
na Rais Magufuli hayana Budi kuweka kwenye Historia.
" Ili wajukuu zetu hapo
badae waweze kujua Rais wa awamu ya Tano alifanya mambo gani mazuri katika uongozi
wake.’’, amesema Majaliwa.
Waziri Mkuu huyo alisema kuwa
Rais Dkt. Magufuli ametoa salamu kwa wananzuoni hao na kuwapongeza kwa kazi
nzuri waliyofanya yenye lengo la kuelimisha jamii kwa shughuri za maendeleo
zilizofanywa na Serikali ya wamu ya Tano.
Nimejaribu Musoma kidogo kitabu hiki lakini ni ukweli usiopingika kimeonesha taswira ya uongozi mahiri wa Serikali ya awamu ya Tano ambayo imefanya mambo mengi mkaubwa kwa muda mfupi, huku nidhamu Serikalini ikiwa kwa kiwancha juu
Kassim Majaliwa.
Kufuatia umuhimu kitabu hicho
Waziri Mkuu ameatoa agizo nakala 100 zipelekwe katika Vyuo Vikuu na
vya kati ili wanafunzi waweze kusoma na kujifunza aina ya uongozi
bora katika kulitumiakia Taifa.
Aidha Waziri Mkuu huyo pia
aligiza nakala 3000 zisambazwe katika Wizara mbalimbali, Wakuu wa
Wilaya, Mikoa pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri wavisome na kujifunza namna
bora ya uongozi uliotukuka.
Majaliwa amesema kitabu hicho
kilichoandika mambo makubwa ya maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya
Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kuanzia 2015 hadi 2020 kimetoa majibu
kuhusu kukua kwa Uchumi, Kodi, Biashara, Mazingira Maji, Afya Elimu pamoja na
utekelezaji wa irani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Aidha Waziri Mkuu amesema
mbali na mazuri ya Serikali ya awamu ya Tano lakini wanzuoni hao
hakusita kuandika mabaya yanayofanywa na watu wasioitakia mema nchi hii, kwa
kutoa taarifa mbaya za uongo kupitia vyombo vya habari za nje ya nchi, lengo
ikiwa ni kuichafua Serikali na viongozi wake wa juu.
‘’Maudhui ya kitabu hiki ni
utekelezaji wa Irani ya CCM, ikiwemo kuvutia uwekezaji katika sekta
mbalimbali.
"Ilikitabu hicho kiweze
kuwafiki wananchi wengi Waziri Mkuu aliagiza kitabu
hicho kuchapishwa nakala nyingi tena kwa lugha ya
Kiswahili kwa kitabu hicho kimetoa ushauri viongozi kufanya kazi na wananchi
kwa karibu," amesema.
Aidha waziri Mkuu alijibu ushauri
ulitolewa katika kitabu hicho wa kuhimarisha uwekezaj na kuondoa kero
mbalimbali zinazowakabili na rushwa ambapo amesema mauala hayo
yanaendelea kufanyiwa kazi ili kutatua changamoto zake.
‘’Kitabu hiki nitakifikisha kwa
Rais Dkt. Magufuli kwania kimesheni mambo muhimu yanayisadifu muelekeo ya
KIuchumi wa Nchi yetu’’, amesema Waziri Mkuu.
Naye Prof Mallya mkono ambaye
ndiye Mhariri Mkuu wa Kitabu hicho amesema kuwa anashukuru kazi
waliyoianza ya kuandika kitabu hicho imekamilika na jana
kufanikiwa kukizindua na Waziri Mkuu.
Mallya mkono amesema
walianza kuandika jinsi Rais Dkt. Magufuli alivyoanza kazi na kuikuta nchi
ikiwa katika hali ngumu kwani alianza kusafisha mafisadi, kusikitisha mkataba
wa fukwe ya Bagamoyo na kubadili mikataba ya Madini iliyokuwa kandamizi kwa
Taifa.
Aidha Profesa huyo amesema
Serikali ya Rais Dkt. Magufuli ilianza kufanya miradi mikubwa ya kujenga
miundombinu katika sekta mbalimbali lakini baadhi ya viongozi wa
Vyama vya Upinzani walioonesha kutokuwa na Uzalendo.
‘’Kuna kiongozi mmoja wa Chama
cha Upinzani alienda huko Ughaibuni akaongea na chombo kimoja cha
nje kuwa Serikali imeua watu 300, akaulizwa na huyo mtangaji una uhakika
akajibu sina, hapo ndio ilioonesha wazi mtu anatumia uongo kuichafua nchi’’,
amesema Mallyamkono.
Prof, Mallya amesema, suala la
Colona, ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR,Bwawa la Mwalimu Nyerere, sifa ya kupiga
vita ufisadi, rushwa, na Uchumi kupanda kwa asilimi 48 hayo ndio
iliyowafanya kuandika kitabu hicho.
Tumeona Magufuli ndio mtu ambaye Watanzania walikuwa wakimuhitaji kwa miaka mingi wakitaka mbadailiko hivyo Rais Magufuli ndio Mwanamabadiliko waliyekuwa wakimsubiri
Prof Mallya
Naye Waziri wa Ardhi Willium
Lukuvi akichangia mjadala huo amesema kuwa alichokifanya magufuli kwa miaka
mitano iliyopita sio kigeni kwani alionesha uwezo tangu alivyokuwa Waziri wa
Ujenzi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony
Mtaka alimpongeza Prof Mallyamkono na wenzake kwa kutambua kuwa Rais
Dkt. Magufuli ni mwanamageuzi wa kwanza kama jina la kitabu linavyosema.
0 Comments