📌SALEH RAMADHANI.
Amesema matokeo yanaonyesha kuwa baadhi ya maeneo hapa nchini bado
yanachangamoto ya ugonjwa huo hasa maeneo yanayozunguka kanda ya ziwa huku idadi kubwa ya Watoto wenye umri chini
ya miaka mitano wakiadhirika Zaidi.
"Ugonjwa wa kichocho bado ni changamoto kubwa
katika maeneo ya ziwa victor,ziwa Nyasa na ziwa Tanganyika,idadi kubwa ya watoto na watu wenye umri wa kati hadi
miaka 55 waliopimwa katika Eneo la Ukerewe wameathirika katika sehemu kubwa na
Tafiti kama hizi zinatuamsha sisi watekelezaji wa mifumo ya Afya na
Matibabu" Amesema
Kufuatia hilo amezishauri mamlaka zinazohusika
ikiwemo Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) kwakuwa
wao wana mamlaka makubwa kufika katika maeneo yaliyoathirika kuona namna ya
kusaidia kuwatibu ilikuokoa vifo vingi ambavyo vinaweza kutokea.
"Nizishauri Mamlaka husika kama ofisi ya Raisi
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) ambao ndiyo watekelezaji wakubwa
katika maeneo ambayo yanamadhara makubwa hata katika bajeti zetu tuzipange
vizuri ili tuweze kuwaokoa watoto wasiende kuwa na madhara ya muda mrefu na pia
tutaokoa vifo vingi" Amesema
Naye Mkurugenzi wa kuratibu na kukuza utafiti NIMR
na mtafiti kiongozi wa mradi wa tiba Dokta Paul Kazyoba amesema wameamua kufanya utafiti juu ya
ugonjwa huo baada ya kuna haupewi kipaombele kama magonjwa mengine na kubaini
kuwa Watoto chini ya umri wa miaka mitano wanaathirika Zaidi hasa katika wilaya za nyasa na ukerewe.
"Katika mkutano wetu tumeangalia ukubwa wa
tatizo la kichocho kwa watoto umri chini ya miaka mitano,ni moja ya Tafiti
ambazo zipo kwenye Mradi wa Tiba na Matokeo yake yapo Tayari kufanyiwa Kazi ili
kuondoa Tatizo la kichocho nchini" Amesema kazyoba.
0 Comments