📌HAMIDA
RAMADHAN
WAZIRI wa Nchi Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka Wakuu wa Mikoa
hapa Nchini kuwa walezi wa shule za Ufundi ili kufanya mabadiliko na
Mapinduzi makubwa ya viwanda.
Waziri Jafo
ameseyasema hayo leo Jijini hapa wakati alipokuwa akiongea na walimu
wapya na Wakuu wa Mikoa kupitia njia ya Mtandao ambapo amewataka walimu kuacha
kujifungia na badala yake wawashirikishe mafundi mahili waliopo mitaani ili
kuleta Mapinduzi ya viwanda kwa wanafunzi na shule zote za ufundi.
Waziri Jofo amesema
shule za ufundi kipindi cha awali zilipoteza hadhi yake na hapakuwa na
miundombinu Wala rasilimali Watu Hali za shule hizo zilikuwa mbaya.
"Shule za ufundi
zinawaandaa Vijana kujifunza masuala ya ufundi
Hivyo basi niziagize
Halmashauri zote zisimamaie miondombinu ya shule hizo na kuzikarabati kila
wakati," amesema Waziri Jafo.
Aidha amefafanua
kwamba jumla ya Shilingi bilioni 16.34 zimetengwa na Serikali kwa ajili ya
ukarabati wa shule zote za ufundi ambapo pia jumla ya walimu150 wameajiliwa ili
kupelekwa Katika shule hizo.
"Hivyo basi
Niwaagize walimu wote walioajiliwa waakikishe wanakwenda kufanya kazi kwa bidii
na umahiri Katika taaluma hiyo ya ufundi hatutaki kusikia habari za kununua
Chaki na badala yake shule hizi za ufundi zitengeneze Chaki," .
Na kuongeza kusema
kuwa " Haiwezekani hadi leo bado tunaagiza vijiti vya meno nchini China
hii ni aibu wakati tunamiti ya kutosha kwaajili ya kutengeneza mbao,"
amesema Waziri Jafo.
0 Comments