📌DEVOTHA SONGORWA.
Baadhi ya wakazi wa
jiji la Dodoma wamesema juhudi za wapigania Uhuru wa Zanzibar zinapaswa
kuenziwa kwani ni sehemu ya Zanzibar ya leo.
Kufuatia Zanzibar
kupata Uhuru wake kumeijengea uwezo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika
kutoa huduma bora za Kijamii kwa Wananchi wote bila ya Ubaguzi.
Wakizungumza jana na
mtandao huu ikiwa ni maadhimisho ya miaka 57 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar
ambayo hufanyika kila mwaka yalifanyika katika viwanja vya mnazi mmoja mjini
Zanzibar mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Zanzibar, Dk.Hussein Mwinyi.
Wananchi hao
walieleza kuwa kupatikana kwa Uhuru kumeleta mabadiliko makubwa kwa raia
wenyewe na Taifa kwa ujumla.
Husna Rashid ambaye ni
mkazi wa Mnada Mpya alieleza kwamba miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa
na mageuzi makubwa katika maendeleo kwani waasisi wake waliacha alama ya mfano
katika Taifa hilo ikiwemo amani na utulivu.
"Leo Wazanzibar
Wana amani na utulivu kwa sababu ya walitangulia walihatarisha maisha yao
kukomboa Taifa kutoka kwa watawala niombe tudumishe tunu hii muhimu kwetu na
watumie Maadhimisho haya kwa mrengo chanya,"alisema Husna.
Akizungumzia nyanja ya
maendeleo John Litware mkazi wa Viwandani alipongeza hatua hiyo akisema kuwepo
kwa Uhuru kumeifanya Zanzibar kujitegemea na kujisimamia katika mambo yake ili
kuwaletea wananchi maendeleo.
" Unajua hakuna
maendeleo katika utumwa leo hii Zanzibar inajitawala yenyewe hii inaonyesha
kabisa msingi mkubwa uliojengwa na wapigania uhuru tunaona huduma nyingi
zimeboreshwa ikiwemo afya, elimu,miundo mbinu na ushirikiano mkubwa na Tanzania
Bara,"alipongeza Litware.
Sherehe za Maadhimisho
hayo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu
Hassan,viongozi wa dini na vyama yakiambatana na na shamra shamra
mbalimbali kama hatua ya kuenzi mema yaliyofanywa na waasisi wa Uhuru wa Taifa
hilo.
Mapinduzi ya Zanzibar
yalitokea mwaka Januari 12, 1964 ili kumuondoa madarakani Sultani wa Zanzibar
na serikali yake, iliyoundwa hasa na Waarabu, na hatimaye kuweka uongozi
mikononi mwa Waafrika.
Aidha historia
inaonyesha kuwepo kwa sababu nyingi za kufanyika kwa mapinduzi ya kulikomboa
Taifa hilo kutoka mikononi wa waingereza kiuchumi,kijamii na kisiasa na kupinga
ubaguzi na Sasa ni NChi huru na watu wake.
0 Comments