📌MWANDISHI WETU
NAIBU Waziri wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo Abdallah Ulega amewataka maafisa michezo nchini kuanzisha program za
kukuza vipaji na kuendeleza michezo nchini.
Akizungumza katika ufunguzi wa Kikao kazi cha
Maafisa Michezo kutoka Mikoa yote nchini jijini Dodoma,Ulega amesema matokeo mabovu
yanayotokea katika michezo mbalimbali ni matokeo ya kutokuwa na program
endelevu katika ngazi mbalimbali mikoani.
Watu huwa wanaibuka kulaumu tu siku Taifa Stars ikifungwa lakini hatujiulizi wale wachezaji waliopo pale wamelelewa wapi,tukiwa na msingi mzuri huko chini hata ngazi za juu tutafanya vizuri na Tanzania itatamba katika michezo mbalimbali.
Ulega.
Ulega amesema serikali ya awamu ya tano imedhamiria
kufanya michezo kuwa kipaumbele kwa vile michezo si ajira lakini inabeba furaha
za Watanzania.
Naibu Waziri huyo amewataka maafisa michezo hao kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao na kushirikiana na wadau wengine wa michezo ili kuendeleza na kukuza vipaji ili kutengeneza timu za ushindani zitakazosaidia taifa katika michuano ya kimataifa.
Ulega pia ameweka wazi dhamira ya serikali kupanua
chuo cha Michezo cha Malya jijini Dar es Salaam ili kuongeza idadi ya wataalamu
wa michezo nchini.
Tunahitaji wataalamu zaidi katika tasnia ya michezo,hivyo tawi hilo litatusaidia kupika wataalamu wengi zaidi watakaoleta chachu katika michezo.
Ulega
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Yusuph Singo,amewataka Maafisa hao wa michezo kuanza kuchagua aina ya mchezo mmoja ambao utakuwa ndio kielelezo cha mkoa husika katika michezo mbalimbali ikiwemo UMISETA na UMITASHUMTA
Naibu Waziri Ulega (Katikati Waliokaa) akiwa na baadhi ya Maafisa Michezo kutoka mikoa mbalimbali |
.
0 Comments