📌SALEH RAMADHANI.
Kituo cha utafiti wa mifugoTaliri wilayani
kongwa mkoani Dodoma kimebainisha kuwa endapo wafugaji watatumia mbinu bora za
ufugaji wanauwezo wakujiongezea kipato kikubwa kitakachowapelekea kuishi maisha
mazuri zaidi.
Hayo yamebainishwa na kaimu mkurugenzi
kituo cha utafiti wa mifugo Taliri kongwa DR.wilfred Munisi ambapo amesema kuwa
wafugaji wakibadilika na kufuga kisasa wanauwezo wa kubadili maisha yao kwa
asilimia 70 na kuwataka wafugaji kutembelea vituo vya utafiti wa mifugo nchini
ili kujionea shughuli zinazofanyika katika Taasisi mbalimbali za utafiti ili
kuboresha mifugo yao.
"Tunafanya utafiti wa mifugo ili jamii ya
kitanzania inufaike na ijipatie kipato maana ufugaji ni sehemu ya utajiri
lakini jamii haitambui na sisi kama Taasisi ya utafiti hapa kongwa milango yetu
ipo wazi kwa yule anayehitaji kujifunza namna ya kuboresha mifugo yake"
amesema.
Dr.munisi amesema kuwa hakuna sekta
ambayo inalipa kama sekta ya ufugaji nchini huku akiwataka vijana
kujishughulisha ili kuendana na kasi ya mabadiliko katika sekta ya kilimo na
ufugaji.
"Hivi nyie vijana kwanini msifuge kisasa
ili mnufaike na mifugo yenu mnayoihudumia huko nyumbani,sekta ya ufugaji na
kilimo ni sehemu kubwa ya mafanikio lakini nyie hamtembelei vituo vya utafiti
nchini ili mjifunze namna ya kuboresha mifugo yenu ya asili mnayoihudumia huko
majumbani" amesema.
Kwa upande wake Mtafiti idara ya mbuzi Christopher mtwange amebainisha kuwa mbuzi aina ya gogo white na buchosa wanauwezo wakuzaa mapacha sita hadi watatu endapo mfugaji atamtunza vizuri huku akisisitiza kuwa wanafanya Tafiti nyingi za ufugaji ili kuboresha mifugo na kuleta tija kwa wafugaji.
"Tunafanya hivi ili kuiboresha mifugo
yetu ya asili na mbuzi hawa wanauwezo wa kuzaa mapacha watoto watatu mpaka
watoto sita,mbuzi aina ya gogo white na buchosa wanauwezo wa kuvumilia ukame na
magonjwa,pia mbuzi hao tunawatunza na tunawaongezea thamani" amesema
Naye merchades Rutechura Afisa utafiti
kutoka Tume ya taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH) amesema kuanzia mwaka
2010 serikali kupitia tume ya Taifa ya sayansi na Teknolojia imetumia zaidi ya
shilling billion 50 kufadhili miradi ya utafiti na ubunifu nchini.
"lengo la kufadhili miradi ya utafiti na
ubunifu ni kusambaza hizi tafiti kuwafikia wananchi na zaidi ya miradi ya
tafiti mia moja tayari zimeshafanyika na zimewafikia wananchi, pia tunawaomba
wanahabari kuhabarisha umma kuhusu tafiti zinazofanyika katika taasisi za
utafiti wa mifugo na kilimo ili ziwafikie kwa wakati na wazitumie kwa manufaa
yao na Taifa kwa ujumla" amesema.
Hata hivyo Rutechura amesema kuwa
wamegundua kuna mbegu nyingi za wanyama ambazo zinatakiwa kuwafikia wananchi
ambapo amedai kuwa hiyo ni kazi ya waandishi wa habari kuhakikisha zinafika
katika jamii ili iweze kutambua.
"Waandishi wa habari pelekeni hizi
taarifa za utafiti ili umma utambue mbinu bora ambazo zitawawezesha wengi
kuendana na mabadiliko ya tabia nchi,pia umma ufahamu hizi taasisi za utafiti
na wazitembelee ili wajifunze namna ya kujiongezea kipato kwa kupitia sekta ya
ufugaji na kilimo,pia matokeo haya tunataka yasaidie katika uchumi wa
Taifa kwa sababu kila tunachofanya katika chuo cha utafiti tungependa kiwafikie
wananchi na tunatumia fedha nyingi za Serikali ili zisaidie hizi teknolojia na
kurahisisha maisha ya mtanzania,”amesema.
Tume ya taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH) iliandaa mafunzo ya siku mbili kwa Waandishi wa Habari wa Mikoa ya Dodoma na Singida pamoja na watafiti na kwa siku mbili waandishi wa habari walipata fursa ya kutembelea miradi mbambali pamoja na watafiti katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo (Tari Makutupora),Taasisi ya Mifugo (Taliri Kongwa) na (Taliri Mpwapwa).
0 Comments