📌DEVOTHA SONGORWA.
WAZIRI wa Kilimo, Profesa, Adolf Mkenda, amekabidhi magari matano na komputa 70 kwa warajisi wa mikoa lengo likiwa kuendeleza vyama vya ushirika na kuimalisha utendaji katika vyama hivyo.
Makabidhiano
hayo yamefanyika leo januari 06,2021 katika viwanja vya Tume ya Maendeleo
ya Ushirika Tanzania (TCDC),jijini Dodoma.
Waziri
Nkenda amesema serikali imedhamiria kurudisha heshima na imani iliyokuwa
imepotea kwa ya watu kutokana na madhaifu ambayo yamekuwa yakijitokeza
kama wizi, ubadhirifu wa mali za umma na mfumo mbovu wa uongozi kwenye vyama
hivyo.
Amesema
anatambua kazi kubwa inayofanywa na vyama vya ushirika ikiwa ni pamoja na
kuunganisha nguvu katika sekta ya uzalishaji ikiwemo kuwasaidia wafanyabiashara
wadogo kama wavuvi na wakulima.
"Tunataka
kuhakikisha ile heshima ya mwanzo inarudi ili watu wengi hasa wakulima kujiunga
na vyama vya ushirika na kukuza soko letu la mazao kimataifa," alisema
Profesa Mkenda.
Amesisisitiza
kumekuwa na baadhi ya watu ambao wanaichafua taswira ya vyama vya ushirika
kutokana na wizi na utendaji mbovu wa kazi, hivyo aliwataka viongozi kwenda
kushughulikia changamoto hizo.
Amesema
serikali itahakikisha inashirikiana vyema na vyama vya ushirika ikiwa ni pamoja
na kupitia upya sheria ya vyama hivyo ili kuona ni sheria zipi zinakuwa kikwazo
kwa baadhi ya watu kushindwa kujiunga.
“Tutapitia
upya sheria ya vyama vya ushirika pamoja na kukomesha wizi na ubadhirifu ili
kuhakikisha unakwisha kabisa," alisema.
Naye,
Mrajisi wa Vyama vya Ushirika ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo
ya Ushirika Dk. Benson Ndiege, alimshukuru waziri huyo kwa kukamilisha
makabidhiano hayo na kumuomba aendelee kutembelea taasisi hiyo.
Ndiege amesema tume inaendelea kuhamasisha wanachama wa vyama vya ushirika, kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za vyama vyao na wakati huo akiwahamasisha viongozi kuendelea kutoa huduma zinazotarajiwa na wanachama wao.
Amesema
wanaendelea kuimalisha ushirikiano na taasisi zingine za serikali, binafsi na
wadau wa ushirika katika kuongeza thamani kwa wanaushirika.
“Ili
kufanikisha yote haya tutahakikisha vyama vinapata viongozi wenye uwezo na
weredi kwenye vyama vya ushirika na tutashirikiana na na taasisi zingine za
serikali kuazia mikoa ,wilaya mpaka Takukuru,”alisema.
Ndiege
amesema katika kuhakikisha wanadhibiti wizi na ubadhirifu katika vyama hivyo,
alisema wamejipanga kuhakikisha wanafanya usimamizi wa mara kwa mara kwenye
vyama vya ushirika na kuhakikisha wale wote wanaojihusisha na wizi au
ubadhirifu wa mali za ushirika wanawajibishwa ipasavyo.
“Tumejipanga
kisawa sawa kuhakikisha kila sekta inakuwa vizuri hatutafumbia macho vitendo
vyovyote viovu vitakavyo jitokeza, tupo tayari kufanya kazi na yeyote atakayekiuka
maagizo ya tume,” amesema.
Magari manne yaliyokabidhiwa leo Januari 06,2021kwa warajisi na Waziri wa Kilimo, Profesa, Adolf Mkenda kwa warajisi wa mikoa lengo likiwa kuendeleza vyama vya ushirika na kuimarisha utendaji katika vyama hivyo.
0 Comments