SERIKALI YAANZA KURUDISHA MIUNDO MBINU YA MADARAJA MPWAPWA.



📌
STEVEN NOEL-MPWAPWA. 


UONGOZI wa halmashauri ya  wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma umeanza kujenga daraja liliko kuwa limebomoka kufuatia mvua za mwaka 2020.

Daraja hilo lililo kuwa kiongo muhimu cha mji wa Mpwapwa katika ya mtaa wa National Hosing na mjini kwa ajili ya shughuli za kibinadamu. 

Akiongea na mwandishi wa habari ofisi kwake  meneja wa TARULA wilaya ya Mpwapwa Mwandisi  Emanuel Lukumay alisema serikali imeamua kuishughulikia changamoto ya daraja lililokuwa limebomoka kufuatia mvua ilionyesha mwaka jana hivyo watarudisha  mawasiliano na kuunganisha mji wa Mpwapwa uliokuwa umeganyika. 


Alisema  sasa daraja hilo linajegwa na Kampuni ya Tecnics contraction  ya mjini Dodoma. "Kampuni inayojenga daraja hili ni kampuni ya kizawa kutoka Dodoma na daraja linagharimu shilingi million 972,370,287.50/= na kwa mujibu wa mktaba ni siku 180 ambayo Sawa na miezi sita. kukamilika kwake "aliongea. 

Msimamizi wa Kampuni ya Tecnics kutoka mjini Dodoma  bwana  George Ndule alisema kampuni yake iliingia mkataba wa ujenzi wa daraja hilo  November 27mwaka 2020  na wanategemea kukabithi kazi ya ujenzi wa daraja hilo mwanzoni mwa mwezi Mei 2021.

Aidha alisema ujenzi wa daraja huo umefikia hatua ya asilimia 50 na kazi inaendelea "japo changamoto za maji kidogo Ndio inaturudisha nyuma tungekuwa tumefika zaid ya asilimia hizo tulizo jenga "aliongea 

Bwana Ndule alisema daraja hilo litawezesha magari mawili kupishana na wavuka kwa miguu watakuwa na sehemu yao ya kupita.

Mmoja wa wananchi wa Mpwapwa Ahmad Bakari alisema kukamilika kwa daraja hilo kutapunguza adha iliyokuwapo kwa wananchi kupita njia ndefu na hivyo kusababisha usimbufu. 

Alisema Pia kuvunjika kwa daraja hilo kulikuwa kunatishia usalama wa  maisha ya watoto wadogo na wazee ambao ilikuwa inawalazimu kupita humo humo korongoni  na kutishia usalama wao hasa kipindi hiki cha mvua. 

Post a Comment

0 Comments