📌MWANDISHI WETU.
Waziri
wa Maji Mh.Juma Aweso amesema Serikali inaendelea na jitihada mbalimbali
kuhakikisha kuwa inaondoa tatizo la Maji katika maeneo mbalimbali ikiwemo jiji
la Dodoma
Waziri
Aweso ameyasema hayo Wilayani Chamwino
Mkoani Dodoma wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa
Miradi
mbalimbali inayotekelezwa Mkoani Dodoma ikiwa ni pamoja na ujenzi wa tanki la
maji litakalokuwa na uwezo wa kuhudumia eneo zima la Chamwino Ikulu, na mradi
wa kuchimba visima eneo la Ihumwa jijini Dodoma.
"Tunajua
kabisa ni lazima tuongeze uzalishaji kwenye mfumo,tuna mpango wa kuchimba
visima vidogo vidogo kumi,na hadi sasa tumekwisha chimba saba,lakini pia
tunachimba visima vikubwa vitatu tumekwishaanza na vikikamilika vitaongeza Maji
Lita Milioni 21 na Maji haya tutaongeza kwenye mfumo ili kuhakikisha wananchi
wanapata huduma hii muhimu ya Maji" Jumaa Aweso,Waziri wa Maji
"Sisi
kama Wizara pia tuna Mikakati mikubwa ya kuhakikisha tatizo la maji linakuwa
historia,Dodoma kila siku watu wanaongezeka na sasa baada ya kuyatoa maji Ziwa
Viktoria kuyapeleka Igunga,Tabora mpaka Nzegani muda sasa wa kuyatoa maji huko
na kuyaleta hapa Dodoma ili wananchi wa hapa wapate huduma ya maji"Alisema
Vile
vile amemtaka mkandarasi anayetekeleza
ujenzi wa tanki kubwa la maji kata ya Bwigiri Chamwino, ambaye ni shirika la
uzalishaji mali la Jeshi la kujenga taifa SUMA JKT kuhakikisha anaongea nguvu
kazi katika eneo hilo ili ujenzi wa tanki hilo ukamilike ndani ya mda aliopewa.
"Mnaposema
mnafanya kazi usiku na mchana tunataka tuone kweli kazi inafanyika usiku na
Mchana,lakini ukiangalia hapa kuna Taa moja tu,hiyo kazi inafanyikaje usiku?,
watu wa Suma JKT kwanini wasiongeze wafanywkazi wakati hawatudai fedha?,kwa
nguvu kazi hii tutachelewa"Aliongeza Aweso
Amesema
hajaridhishwa na kasi ya ujenzi huo kutokana na nguvu kazi ndogo katika eneo
hilo na kuhofia kufika mda na ujenzi wa tanki hilo ukawa haujakamilika.
Vile
vile Amemtaka msimamizi wa mradi huo Mhandisi Kashilimu Mayunga kuhakikisha
anasimamia kazi hiyo mchana na usiku na kuhakikisha kila mahitaji
yanayohitajika katika mradi huo yanapatikana kwa wakati na mradi kukamilika kwa
wakati uliopangwa.
0 Comments