MWENYEKITI CTF ATOA WITO KWA WASABATO.



📌FAUSTINE GALAFONI.

Katika kuadhimisha siku 10 za Maombi,Mwenyekiti wa kanisa la Waadventista Wasabato jimbo la Kati mwa Tanzania[CTF]Mchungaji Toto Bwire  Ndege Kusaga ametoa wito kwa Washiriki wa Kanisa la Waadventista Wasabato katika jimbo hilo kuendelea kuhudhuria kwenye vituo  vya ibaada  kwa ajili ya kufanya maombi .

Mchungaji Kusaga amebainisha hayo  leo Januari,7,2021 wakati akizungumza na Mtandao huu jijini Dodoma ambapo amebanisha kuwa Mungu huwa hashindwi hata kama utakuwa na jambo gumu namna gani hivyo ni vyema kila Mshiriki kutumia siku 10 hizi za Maombi kujinyenyekeza kwa BWANA kwani hujibu kila hitaji .

Mchungaji anayemaliza Muda wake katika  Mtaa wa chuo kikuu cha Dodoma [UDOM]Mchungaji  Johnson Chilagi amesema Siku 10 za Maombi katika mtaa huo zimeendelea vizuri ambapo takriban zaidi ya Wanachuo  elfu moja na mia tano[1500] wanashiriki  huku idadi ikitarajia kuongezeka zaidi na akibainisha kuwa ratiba za Masomo za Chuo hazijaingiliana na Muda huo wa maombi.

Elias  Maiga Aroun ni Mzee wa Kanisa la Waadvetista Wasabato Kikuyu jijini  Dodoma ambapo amebainisha kwa siku ya kwanza  takriban Washiriki 50 walihudhuria katika siku 10 za Maombi kanisani  hapo huku Mwinjilisti Kutoka kanisa la Waadventista Wasabato Ndachi Stra Pheneas akibainisha kuwa wanashiriki kuombea amani,wafungwa pamoja na neema ya BWANA kuzidi kubariki zaidi.

Kwa mujibu wa Kalenda ya Kanisa la Waadventista Wasabato Ulimwenguni[General Conference],kila ifikapo  Mwezi Januari ya kila Mwaka huwa zinatengwa siku maalum 10 za Maombi ambapo mwaka jana zilianza  tarehe 8 hadi 18 mwezi Januari  na Mwaka huu    zimeanza Tarehe 6 hadi Tarehe 16,2021

Post a Comment

0 Comments