📌MUHAMMED KHAMIS.
Baadhi ya Wananchi wa Shehia mbali mbali Unguja wameleza matarajio yao juu ya ujio wa mradi wa Viungo kuwa utakwenda kufungua fursa kwa wakulima pamoja na kuongeza kipato sambamba na upatikanaji wa lishe bora na uwekaji wa hakiba dhidi yao.
Wameyasema hayo katika
shehia ya Bandamaji mkoa wa kaskazini Unguja na baadhi ya shehia nyengine mbali
walipokua wakipatiwa elimu juu ya mradi huo utakao jikita katika kilimo cha
matunda,mbogamboga pamoja na viungo na kufanyika zaidi ya shehia 50 za Unguja
na Pemba.
Wamesema kwa miaka
mingi wamekua wakijishughulisha na shughuli za kilimo tofauti lakini hadi leo
hii bado hawajafikia malengo yao ipasavyo.
Mmoja miongoni mwa
wananchi hao Kidume Juma amesema licha ya kuwa shughuli kubwa kwao ni
kilimo lakini hadi leo hii bado wakulima walio wengi wamebaki kuwa masikini
wanati wao ndio walipaswa kuwa kama walivyowakulima wengine ulimwneguni.
Amesema imefika wakati
wakulima katika eneo hilo na maeneo mengine wanafanya shughuli hizo kama mazoea
lakini si kwa kutegemea mafanikio kama wengine.
Nae Chapa Mkali Juma amesema licha ya uwepo wa changamoto hio lakini pia wamekua wakikabiwa na tatizo kubwa la uhaba wa masoko kwa bidhaa zitokananzo na kilimo chao.
Amesema katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar wananchi walio wengi hususani mashinani vijijini wamehamaisika na kilimo lakini wamekua wakikata tamaa wanapoona bidhaa zao zinakwenda sokoni bila kununuliwa kama walivotarajia.
Ameeleza kuwa kikawaida mkulima hutumia nguvu nyingi kuzalisha mazao lakini matunda ya nguvu hizo ni madogo sana na yasioendana na uhalisia wa kazi wenyewe.
‘’Kwa mfano ulanguzi unaofanywa na baadhi ya watu masokoni wanaojiita madalali kushusha bei kwenye mazao yetu kwa sababu tofauti ikiwemo kukosa ubora wa bidhaa huku wao wakiuza bei za juu kwa wanunuzi suala hili linatuumiza sana na lazima lifanyiwe kazi’’ameongezea.
Akitolea ufafanuzi wa changamoto hizo afisa Afisa maendeleo biashara kutoka mradi wa viungo Zanzibar Mwanaidi Mussa Shembwana alisema katika jamii kumekuepo na wakulima wengi wanaoendelea kulalamikia kukosa manufaa ya jasho lao kutokana na sababu tofauti.
Akitaja miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na wakulima kutojua mbegu sahihi za matunda ambazo zingeweza kuwasaidia kupata kipato zaidi kufuatia uhitaji wa wananchi sokoni.
Amesema kwa mfano hadi leo hii katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar licha ya kuwa ardhi yake kukubali kilimo cha nanasi lakini bado wakulima hawana taaluma ni aina gani ya matunda hayo yanahitajika zaidi katika masoko ya ndani na ya kimataifa.
Sambamba na hayo
amesema wakulima wanahitaji kupatiwa elimu ni wakati gani na sahihi kwao
kufanya kilimo na mbegu gari ni bora zaidi kwa kuwa kuna mazingira
kikawaida si sahihi kuazisha baadhi ya vilimo kutokana na kukosa uhitaji wa
bidhaa katika kipindi hicho.
Kuhusu suala la uhaba
wa masoko aliwataka wakulima hao kuamini kuwa kila bidhaa iliobora inauzika
sokoni hivyo kupitia mradi huo watahakikisha wanufaika wote wale iwe wa vikundi
au mtu mmoja mmoja wanazalisha bidhaa bora na zenye viwnago vya kimataifa.
‘’Kwa hili la masoko
naomba niwatoe wasiwasi tuna wenzetu ambao wapo Canada jukumu lao kwa
kushirikiana na sisi nikuhakikisha tunapata masoko ya kimataifa kwa bidhaa zote
zinazozalishwa Zanzibar kupitia mradi huu na ninaamini mutaweza’’aliongezea.
Awali afisa fedha kupitia mradi huo Agnes Nicodemas Msengi amesema licha ya mradi huo kunufaisha wakulima kupitia kilimo lakini pia utasaidia wakulima kuwa na utaratibu maalumu wa kujiwekea akiba.
Amesema kuna mkakati maalumu wa taaluma ambayo watapewa wakulima wote hususani wenye vikundi vya akinamama waweze kuweka akiba ya kujipatia mikopo katika benki mbbali mnali hapa Zanzibar.
Mradi wa huu wa viungo ni wa miaka mine na unaendeshwa na taasisi ya People development forume,Community forest in Pemba pamoja na TAMWA-Zanzibar kwa kuufadhiliwa na umoja wa Ulaya chini ya usimamizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
01.Baadhi ya washiriki
wa mkutano wa utowaji elimu kuhusu mradi wa Viungo katika shehia ya Bandamaji
mkoa wa kaskazini Unguja wakifuatilia taarifa za utolewaji wa elimu kuhusu
kilimo cha mboga mboga na matunda pamoja na viungo.
Picha ya pamoja kwa washiriki wa mkutano wa utolewaji elimu dhidi ya mradi mpya wa viungo unaofadhiliwa na umoja wa Ulaya (EU) kwa usimamizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Miongoni mwa washiriki wa mkutano wa utolewaji elimu kuhusu mradi wa viungo ambao ni vijana wakifuatilia kwa makini elimu juu ya mradi huo na umhimu wa ushiriki kwa vijana katika mradi huo.
0 Comments