📌STEPHEN NOEL (MPWAPWA).
WANANCHI wa wilaya ya
Mpwapwa mkoani Dodoma wametakiwa kuchangamkia fursa ya upandaji wa
zao la korosho ambalo linatarajiwa kuwa mkombozi wa uchumi wa wilaya hiyo na kukuza kipata kwa mtu
moja moja.
Shekimweri amesema Serikali haitoacha kuhamasisha zao la korosho ambalo ni zao la kimkakati katika wilaya ya Mpwapwa ili kuinua uchumi wa wananchi.
Ukweli kuanza kitu kipya kinachangamoto zake wapo waliotikia toka mwanzo na wengine wanasita sita hivyo wakioshaona wenzao wamenufaika ndo na wao watajiingiza katika kilimo hicho.Jabir Shekimweri
Aidha Shekimweri amewaagiza maafisa ughani na viongozi wote ngazi ya Kata na vijiji kuhamasisha upandaji wa korosho katika kipindi hiki cha mvua.
Kwa upande wake afisa kilimo anaeshughulikia zao la Korosho wilayani Mpwapwa Edson Kileo amesema, tafiti zinaonyesha kuwa hali ya hewa ya wilaya ya Mpwapwa ni rafiki kwa zao la korosho na linafanya vizuri.
Zao hili hustawi vizuri sehemu zenye mvua ya wastani kiasi cha milimita 800 mpaka 1,600 kwa mwaka kwa wilaya ya Mpwapwa ndicho kiasi cha mvua kinachoweza kupatikana kwa mwakaEdson Kileo
Aidha ameongeza kuwa korosho ni zao la kimkakati katika mikoa ya kanda ya Kati ambalo litaweza kubadilisha maisha ya wananchi wengi wa Mpwapwa na uchumi wa wilaya kwa ujumla.
Mmoja wa wakulima wa zao hilo Suzana Mosha amesema kwa sasa wameanza kuvuna mavuno ya awali ya zao hilo na linaonyesha kufanya vizuri.
Naye Jemsi Senyegalo
amesema pamoja na wananchi kuitikia kwa wingi upandaji wa zao hilo idara ya
kilimo inapaswa kushughulikia changamoto za upatikanaji wa viwatirifu kwa wakulima ili
wavutiwe kujiingiza katika kilimo cha zao la korosho.
0 Comments