📌MWANDISHI WETU.
Mbunge wa Viti Maalum UWT (watu wenye ulemavu) Mhe.Stella Ikupa ametekeleza ahadi yake ya kukabidhi vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu ambapo ametoa jumla ya Baiskeli za watu wenye ulemavu 10 zenye thamani ya hela za Kitanzania milioni nne(4,000,000).
Mhe.Ikupa amekabidhi Baiskeli kwa kijana Marcos Venas aishie kata ya Kimara ambaye aliahidi kumsaidia kijana huyo hivyo ametekeleza ahadi yake kwake,Mama wa Kijana huyo ametoa shukrani kwa Mhe.Ikupa na Uongozi mzima wa Chama Cha Mapinduzi chini ya Mhe.Rais Dkt.Magufuli kwa kuonesha kweli ni wenye kutekeleza ahadi zao kwa haraka katika kuwajali wananchi wote.
Pia Mhe.Ikupa amekabidhi Baiskeli 3 kwa kituo cha kulea watoto wenye ulemavu kiitwacho SALT kilichopo kata ya Mbezi ambapo awali alitoa ahadi ya kumsaidia mtoto mmoja aliyekuwa na uhitaji wa baiskeli hiyo siku ya tarehe 13 mwezi Disemba mwaka jana katika Bonanza la michezo la lililokuwa limelenga kusaidia katika uwezeshaji wa kupata vifaa saidizi ambapo amekamilisha ahadi hiyo na kuongeza baiskeli 2 za ziada kwa kituo hicho,
Mkurugenzi wa kituo hicho Bi.Rebeca Leby ametoa shukrani kwa Mhe.Ikupa kwa juhudi zake katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wenye uhitaji wa vifaa saidizi wanapata ama kuwezeshwa katika kupata vifaa hivyo.
Aidha Mhe.Ikupa amekabidhi baiskeli moja kwa mtoto Salome Asumwike wa Darasa la pili katika shule ya msingi Kalakata ambaye analelewa na Bw.Axon na Bi.Sophia ambao wamemshukuru Mhe.Ikupa kwa kukamilisha ahadi yake ya kumsaidia kijana huyo katika kumpatia baiskeli hiyo ya kumuwezesha kusogea sehemu moja hadi nyingine.
Mhe.Ikupa aliahidi kushirikiana na waheshimiwa madiwani akiwemo diwani wa viti maalum Mhe.Magreth Cheka kuwezesha kujenga choo kitakachokuwa rafiki na wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya Karakata. Tatizo hili lilielezwa kwa mbunge Ikupa kuwa mtoto Salome anapata shida sana akiwa shuleni kwani hakuna kabisa choo rafiki katika shule ya Karakata
Pia Mhe.Ikupa ametekeleza ahadi yake kwa kumkabidhi baiskeli saidizi kijana Andrew Sajusi mkazi wa Yombo vituka ambapo amefuatana na Mhe.Mariam Mbunge wa Viti maalum ambaye ndiye aliyemtambulisha kijana Sajusi kwa mhe.Ikupa
Pia Mhe.Ikupa amempatia mtoto Iddy Halid baiskeli saidizi mkazi wa kata ya Tabata ambapo Mama mlezi wa mtoto huyo Bi.Zainabu amemshukuru Mhe.Ikupa kwa kutimiza ahadi hiyo lakini kwa kuonesha utu na upendo wa hali ya juu pamoja na kujituma kwake katika kusaidia watu wenye ulemavu.
Zoezi hili liliendelea katika kata ya Majohe, Mhe.Ikupa alikutana na watu wenye ulemavu na wazazi wa watoto wenye ulemavu wapatao 140 akiwa amefuatana na waheshimiwa madiwani wa viti maalum watokao Jimbo la Ukonga ambapo ametoa baiskel 2, pampasi na nepi kwa watoto wenye ulemavu.Mhe.Ikupa ameahidi kuongeza baiskel zingine tano katika kata hii ya Majohe na 1 katika kata ya Tabata.
Mhe.Ikupa alitoa ufanunuzi kuwa zoezi hili ni endelevu kwa nchi nzima" zoezi hili litakuwa endelevu kwa nchi nzima, ninategemea panapo uzima nitaendelea kutoa baiskel, bajaji, pikipiki, mafuta ya ngozi kwa watu wenye ualbino n.k".Katika mkutano huu alipokea changamoto mbalimbali za watu wenye ulemavu, ikiwemo uhitaji wa miguu bandia ambapo aliwaelekeza wajiandikishe wahitaji na yeye atawapeleka kwa wadau wanaotoa miguu hiyo.
Pia aliweza kuahidi kumnunulia brenda mama mwenye mtoto mwenye ulemavu ambaye hawezi kula vyakula vigumu
Katika zoezi hili baiskel 1 ilitolewa kwa mtoto mwenye ulemavu Mkoani Morogoro.
Katika zoezi hili la utekelezaji wa ahadi,Mhe.Ikupa pia ameongozana na uongozi wa UWT kata zote katika maeneo yote aliyofika.
0 Comments