📌LUCY NDALAMA
LICHA ya kwamba visa vya ugonjwa wa COVID19
vinavyosababishwa na virusi vya corona kuonekana kuisha nchini Tanzania tangu
mwezi Mei mwaka huu,tahadhari ya ugonjwa
huo na mengine ya mlipuko bado yanahitajika kuchukuliwa.
Makala hii inaangazia sababu kadhaa zinazoweza
yafanya maeneo ya vijijini kuwa hatari zaidi kwa magonjwa ya milipuko ikiwemo
COVID-19.
IDADI
KUBWA YA WAZEE
Tanzania ikikadiriwa kuwa na wazee zaidi ya milioni 2
ikiwa ni zaidi ya 5% ya Watanzania wote na zaidi ya 80 ya Wazee hao wanaishi
maeneo ya vijijini.
Kulingana na Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa japo
idadi kubwa ya watu walioambukizwa virusi vya corona ni vijana wa kati ya umri
wa miaka 25 na 39, idadi kubwa ya wanaofariki ni wazee wa miaka 65 na zaidi.
Kwa mujibu wa WHO, asilimia 75 ya vifo milioni 1.5 vya corona ambavyo
vimethibitishwa kote duniani kufikia sasa, ni wazee wa umri wa miaka 65 na
zaidi.
Tafiti zinaonyesha kuwa wazee hulemewa zaidi na virusi vya corona kwa kuwa
kingamwili zao ni dhaifu. Aidha, kundi la Wazee wengi ndio husumbuliwa sana na
maradhi kama vile kisukari, shinikizo la damu, ugonjwa wa moyo na mapafu
nakadhalika huwa ni watu wa kuanzia umri wa miaka 65 na zaidi.
Hivyo kundi hili linajikuta lipo ahatarini zaidi kutokana na kwamba miili yao
tayari inashambuliwa na magonjwa mengine,hivyo mwili upata kazi ya ziada ya
kupambana na virusi vya corona.
Watu
wenye umri wa miaka 70 kwenda juu pamoja na watu wenye maradhi mengine wako
hatarini kuambukizwa katika maeneo kama hayo. Watu wanaoonyesha dalili za
maambukizi kama kukohoa na mafua wanatakiwa kukaa nyumbani na kujitenga.
Hata hivyo,utaratibu wa kutoa huduma bure kwa
wazee bado una mapungufu. Wazee walio wengi hasa wa vijijini wanaachwa nje ya
utaratibu wa kupata huduma kutokana na kushindwa kuthibitisha kwamba wana umri
wa miaka 60 na hawana uwezo wa kuchangia gharama hizo (Sera ya Wazee).
UPATIKANAJI
WA TAARIFA
Kutokana na ukuaji wa teknolojia na mabadiliko ya
upashanaji wa habari kundi kubwa la watu wanaoishi vijijini bado wanakosa
taarifa sahahi au kupata kwa kuchelewa taarifa hizo.
Mtandao wa internet ambao kwa sasa ndio unatumiwa na
watu wengi kama njia ya kufukisha taarifa na habari mbalimbali kwa wakati
takwimu zinaonesha umesambaa kwa asilimia 45 tu nchini Tanzania.
Licha ya kwamba idadi ya watumiaji wa internet imeongezeka maradufu katika
miaka iliyopita laikini hali bado sio nzuri katika maeneo ya vijijini ambako
81% hawajaunganishwa na mtandao wa intarnet.
Hivyo hali hiyo huchangia jamii nyingi kukosa
taarifa sahihi kwa wakati ambazo kwa sasa hutolewa zaidi kwa njia ya mtandao.
Watu wanaoishi maeneo ya vijijini tegemeo lao kubwa
kupata habari ni radio na tv ingawa kwa uzoefu baadhi ya maeneo bado mawimbi ya
radio upatikanaji wake ni wa shida na gharama za kununua seti ya televisheni ni
kubwa sana.
UPATIKANAJI
WA HUDUMA ZA AFYA
Upatikanaji wa huduma za afya katika maeneo mengi ya vijijini ni
changamoto,licha ya jitihada za serikali kujenga vituo vya afya zaidi ya 360
katika miaka ya hivi karibuni,kipato duni cha wakaazi wa maeneo ya vijijini na
upungufu wa watumishi wa afya ni kikwazo kikubwa katika upatikanaji wa huduma
hizo.
Maeneo mengi ya vijijini yameonekana kuwa na majengo
ya kutolea huduma za afya lakini upatikanaji wa huduma hizo baadhi ya maeneo ni
kitendawili kinachosumbua wahusika kupata jibu na suluhisho la kudumu.
Magonjwa ya mara kwa mara na ya muda
mrefu, ni hali ya kawaida kwa hususani kwa wazee ambao ndio kundi kubwa
linalopatikana maeneo ya vijijini. Hali hii inahitaji uangalizi na matunzo
maalum ya kitaalam. Pamoja na ukweli huo, huduma za afya hazipatikani kwa
urahisi kwa wazee walio wengi na mara nyingi ni ghali.
UPATIKANAJI
WA MAJI SAFI NA SALAMA
Kunawa mikono mara kwa mara ni moja ya hatua ya awali
ambayo wataalam wa Afya wanashauri ili kujikinga na kuzuia kuenea kwa COVID-19.
Sehemu kubwa ya Ulimwenguni upatikanaji wa maji ni changamoto ya mara kwa
mara kwa mamilioni ya watu na inakadiliwa kwamba zaidi ya asilimia 40 ya idadi
ya watu ulimwnguni wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji.
Ikiwa juhudi za serikali ni kuhakikisha tatizo la maji nchini linakuwa
historia,changamoto za upatikanaji wa maji safi maeneo ya vijijini inaweza
ikawa tatizo kubwa katika mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo
COVID-19. Kuosha mikono yako mara kwa mara ni moja ya mambo ya kwanza ambayo
maafisa wa afya ya umma nchini Nigeria na Shirika la Afya Ulimwenguni
wamependekeza kuzuia kuenea kwa COVID-19.
Ulimwenguni kote, upatikanaji wa maji ni changamoto
ya mara kwa mara kwa mamilioni ya watu ambapo inakadiriwa asilimia 40 ya idadi
ya watu ulimwenguni wanakabiliwa na uhaba wa maji.
Pia upatikanaji hafifu wa maji safi na salama katika maeneo ya vijijini
huwalazimsha wakazi wa maeneo hayo kutumia maji ya visima ambayo hawana uhakika
na usalama wake.Homa za matumbo na kuhara pamoja na kichocho.
UKOSEFU WA VYOO BORA
Kwa mujibu wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Jamii na
Uchumi, hadi asilimia 15 tu ya watu vijijini nchini Tanzania wanaotumia vifaa
bora vya usafi wa mazngira ikiwemo vyoo.Hali hii upelekea milipuko ya magonjwa
ya kuhara ikiwemo kipindupindu.
Ukosefu wa vyoo na matumizi yake husababisha baadhi ya wakazi kujisaidia kwenye
vichaka au vyanzo vya maji ambayo pia hutumiwa na kwa ajili ya matumizi ya
majumbani kama vile kupikia na kunywa.
WAGENI KUTOKA MJINI
Maeneo ya vijijini yamekuwa kimbilio kwa makundi
mengi ya watu kitoka mjini,mfano wafanyabiashara wanasemekana kuwa chanzo
kikubwa cha usambazaji wa magonjwa katika maeneo ya vijijini.
Pia imekuwa kawaida kwa kipindi kama hiki cha
sikukuu baadhi ya watu kurudi makwao kwenda kujumuika na wapendwa wao
kusherehekea sikukuu ya Chrismass na Mwaka mpya.
Kwa hapa Tanzania watu wanaotoka mikoa ya Kaskazini hususani mkoa wa Kilimanjaro wanaonekana kwenda kwa wingi maeneo ya vijini walipozaliwa au kuwaacha Wazee wao hivyo wanahitajika kuwa makini zaidi na kufuata ushauri wa wataalam wa afya hili kulinda wenyeji wake huko anapokwenda.
Kwa kuzingatia hayo yote jamii haina budi kuona haja ya kutilia mkazo kuboresha mazingira ya vijijini ili kuweka jamii zinazoishi maeneo hayo salama zaidi.
0 Comments