📌RHODA SIMBA KATIKA kipindi cha
mwaka 2020/2021 serikali imetenga Sh. Bilioni 298 kwaajili ya mpango wa elimu
bila malipo kwa shule za msingi. Amesema katika
kuhakikisha elimu ya msingi hapa nchini inakuwa bora serikali
itaendelea kuboresha miundombinu ya elimu mashuleni ili kukidhi haja ya
wanafunzi na walimu “Serikali iko makini
kuhakikisha suala la elimu linakuwa mbele zaidi kwa kutoa fedha nyingi kwa
ajili ya maboresho ya miundombinu katika ujenzi wa vyoo,vyumba vya madarasa,
Nyumba za walimu na mabweni,”alisema Amesema mabadiliko
makubwa yamefanyika kwenye sekta ya elimu ya msingi ambayo yamechochewa
na mpango huu wa elimu bure na ujenzi wa miundombinu hivyo ni wajibu wa
walimu kusimamia fedha hizo kufanya kazi iliyokusudiwa Katibu Mkuu
huyo aliweka wazi kuwa Serikali inalaani vitendo vya udanganyifu wa mitihani
na kuwataka walimu wakuu nchini kuendelea kudhibiti vitendo hivyo ili
kuboresha elimu ya msingi. “Ni jambo la
kusikitisha kuona katika ulimwengu huu bado walimu hamuwezi kudhibidi wizi wa
mitihani,tunawakatisha tama wanafunzi wanaojituma,. Amesema “hata ninyi
mtakuwa mashahidi kuwa tatizo la udanganyifu wa mitihani bado lipo na
sereikali suala hili halitalifumbia macho kwani kwa kipindi pekee cha
mwaka jana jumla ya wanafunzi 1065 walifutiwa matokeo ya mitihani kwa
udanganyifu,”alieleza. Kwa upande wake
Mkurugenzi wa elimu Tanzania kutoka TAMISEMI ,Julius Nestory alitumia jukwaa
hilo kuwataka walimu kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya
utumishi wa Umma huku akisisitiza kuwa Serikali hatamvumilia mwalimu
yeyote atakayekiuka agizo hilo. Amesema siku za hivi
karibuni yameibuka matukio ya baadhi ya wafanyakazi wa serikali wasio
waadilifu kusambaza nyaraka za serikali kwenye mitandao ya kijamii na kusema
jambo hilo ni kinyume na tarativu za utumishi wa umma. Nestory amesema
walimu wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii hivyo ni jukumu lao
kuepuka matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii. “Matumizi ya
mitandao ya kijamii hayaepukiki katika ulimwengu huu,lakini mnapswa kutumia
kwa uangalifu bila kuharibu taaluma yenu,” alisema. Awali,
Mwenyekiti wa Umoja wa walimu hao(TAPSHA)Rehema Ramole alisema
mkutano huo utasaidia mafunzo mbalimbali ya uongozi, haki na wajibu wao
na kukabiliana na rushwa. Mwenyekiti huyo
(TAPSHA) ambaye pia ni Mwalimu wa Shule ya msingi Makuburi Jeshini
Ubungo jijini Dar es Salaam alieleza kuwa wao kama wakuu wa shule wanao
wajibu wa kukumbushana na kukemea vitendo vya rushwa na kuendelea kuiunga
mkono serikali dhidi ya kukomesha vitendo vya rushwa na uvujaji mitihani
mashuleni. “Tupo pamoja na
Serikali yetu katika kukuza elimu nchini,Kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni
uongozi na usimamizi makini wa elimu utaimarisha na kuiendeleza Tanzania
katika uchumi wa kati inaonyesha wazi ni kwa jinsi gani tupo tayari kupokea
maagizo yoyote yanayotolewa na serikali yenye lengo la kuinua elimu,”amesema.
|
0 Comments