JESHI LA POLISI DODOMA LATOA ELIMU KWA MADEREVA WA BAJAJI NA BODABODA

 


📌RAMADHAN HASSAN.

JESHI  la Polisi Mkoani Dodoma limewataka madereva wa bajaji na bodaboda kufuata sheria za usalama barabarani pindi  wanapokuwa wanaendesha vyombo hivyo wa moto.

Hatua hiyo imekuja kufuatia Jeshi hilo kufanya msako wa madereva bodaboda na bajaji ambao hawakufuata sheria za usalama barabarani  na kufanikiwa kukamata bajaji 17 na bodaboda 47 zilizovunja sheria.

Akizungumza na madereva hao leo Januari 21 mwaka 2021, wakati akiwapa elimu mara baada ya kufanya makosa hayo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,Gilles Muroto amesema ni muhimu kufuata sheria za usalama barabarani pindi wanapokuwa wakiendesha vyombo hivyo vya moto ili kupunguza ajali na vifo ambavyo baadhi husababishwa na uzembe.

“Tunaliheshimu sana kundi lenu la bodaboda na bajaji sasa mfuate sheria za usalama barabarani bahati yenu hamtembelei katika Hospitali na vituo vya afya muone watu waliolazwa na kufariki kutokana na ajali,ajali na vifo ni vingi fuateni sheria za usalama barabarani mmenisikia?” amesema Kamanda Muroto.

Pia amewataka madereva hao kutowaharibia maisha wanafunzi wa kike kwa kuwatongoza ambapo amewataka   kuwaacha wasome ili watimize ndoto zao.

“Manawapakiza katika vyombo vyenu,Muwe makini wengine,wanambemba mwanafunzi unamfanya mkeo hili hapana.Muwe wasafi mfue makoti nadhani mmenisikia,”amesema Kamanda Muroto.

Kwa upande wake,Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Mkoa wa Dodoma,Boniphace Mbao amesema wataendelea kutoa elimu kwa madereva bodaboda na bajaji lengo nilikiwa ni kupunguza ajali barabarani.

Kamanda Mbao amesema  wameanzisha zoezi la kuzikamata bodaboda na bajaji na kisha kuwapa elimu ambapo alidai wamewakamata madereva 47 wa bodaboda na 17 wa bajaji.

mwisho  

Post a Comment

0 Comments