📌RAMADHAN HASSAN
Timu ya Soka ya Wanawake ya Fountain Gate Princess
imetambulisha jezi yake ya tatu huku ikiweka wazi wadhamini
iliowapata kwa ajili ya kuidhamini timu katika Ligi kuu ya Soka ya wanawake.
Pia imesema mikakati yao ni kushika nafasi ya tatu
katika Ligi kuu ya Soka ya wanawake inayoendelea ambapo
imedai msimu ujao ni lazima ichukue ubingwa wa
Ligi hiyo.
Hayo yameelezwa leo Januari 18 2021 na Mkurugenzi
Mkuu wa Shule ya Fountain Gate Academy,Japhet Makau alipokuwa akizungumza
na Waandishi wa Habari.
Makau amesema Fountain Gate imeamua kuingia kwenye
michezo na eneo la kwanza ni katika mpira wa miguu ambapo amedai walianza na
timu ya wanaume ambayo kwa sasa inashiriki Ligi daraja la kwanza.
Amesema wameingia pia katika Soka la wanawake
ambapo mwaka jana waliinunua timu ya Tanzanite na kwa sasa inaitwa Fountain
Gate Princess ambayo inashiriki Ligi kuu ya Soka ya Wanawake.
Makau amesema Fountain Gate Princess ili
izidi kufanya vizuri ni lazima kuwe na wadhamini wa kuweza
kuiendesha timu hiyo iweze kujiendesha ambapo amewataja wadhamini hao
kuwa ni pamoja ni Kampuni ya Korie Super Rice ya Mkoani Morogoro,UBA Bank,Simba
Nazi, na Jeff Solution ambao watasaidiana na Fountain Gate Academy.
“Ili tuweze kufanya vizuri lazima timu zetu
ziwezeshwe na mfadhili mkuu wa timu yetu ni Fountain Gate Academy kwa timu
zote,ili kuhakikisha tunaimarisha mchezo na vijana wanapata kile ambacho
wanakihitaji tumeendelea kutafuta wadhamini wengine na wamekubali,tunao
Korie Super Rice ya Mkoani Morogoro na tutakuwa tunavaa jezi zenye nembo
hiyo.
“Lakini pia tunao UBA Bank ambao wametoa ofa ya
mchezaji bora wa mwezi pamoja na kila goli,wadhamini wengine ni Simba Nazi ya
Jijini Dar es salaam na Jeff Solution,”amesema.
Mkurugenzi huyo amesema mikakati yao ni kushika
nafasi ya tatu katika Ligi kuu ya Soka ya wanawake msimu huu ambapo
amedai msimu ujao ni lazima ichukue ubingwa wa
Ligi hiyo.
Target yetu tunataka kuwa kwenye top three(nafasi ya tatu) mwaka ujao tutaingia kutaka kuwa mabingwa.
Makau
Katika hatua nyingine,Msemaji wa timu hiyo,Juma Ayo amewataja wachezaji saba wapya waliosajiliwa na timu hiyo kwa ajili ya mikimiki ya Ligi Kuu ya Soka ya wanawake huku akidai kwamba mchezo wa kesho wa ligi hiyo dhidi ya Baobao Queens wamejipanga kuondoka na pointi tatu.
Amewataja wachezaji hao na timu wanazotoka katika mabano kuwa ni Aqwila Gasper (Simba Queens) Stella Wilbart (Simba Queens) Saada Ramadhan (Simba Queens)Merry Masatu(Ruvuma Queens) Anna Ebron (Mlandizi Queens ) Zuhura Waziri (Ilala) na beki wa kulia Madelina Agostino (Ilala).
Amesema wachezaji hao watatumika katika mchezo wa kesho wa ligi kuu ya Soka ya Wanawake dhidi ya Baobao Queens mtanange unaotarajiwa kufanyika katika uwanja wa Fountain Gate Arena Jijini Dodoma.
Wachezaji wote hawa wanatumika katika kikosi chetu kwa sasa ni kizuri na kikosi kimekamilika.Kesho tuna mechi na Baobao Queens ni mechi muhimu sana.Nimeona mitandaoni watu wanasema ni ‘Diarby’ sisi tuna kikosi kizuri waone kesho (Baobab Queens) jinsi ya kupunguza mabao maana tutawafunga,mechi itaanza saa 10 kesho hatutarajii kupata malalamiko yoyote,sisi kama Fountain Gate tupo vizuri tunaelekea kuwafunga.Ayo.
0 Comments