DALADALA WAPEWA SIKU 14 DODOMA

 


📌JOHN BANDA

MKUU wa Wilaya ya Dodoma mjini Josephaty Maganga ametoa siku 14 kwa madereva wa Daladala na wafanyabiashara ndogo ndogo  kujiandaa kisaikolojia ili utakapofika wakati wa kuwahamisha katika stend ya sabasaba wasipate usumbufu

Akiongea kwenye Mgomo wa madereva na makondakta wa daladala uliodumu kwa takribani saa 7 mkuu wa wilaya huyo amesema madai yao ni sahihi na hivyo kwa sababu stendi hiyo ni ndogo yaandaliwe maeneo mengine .

Amesema ameyapokea na kuyakubali malalamiko ya madereva hao na kwamba anawagiza wafanyabiashara na wenye daladala hao kujiandaa ili baada ya wiki mbili jana waweze daladala ziweze kupunguzwa ili kukidhi haja ya stendi hiyo ya Sabasaba

Nimeambiwa kuna maeneo ambayo yalishaanza kuandaliwa na jiji miezi zaidi ya 8 iliyopita kule Makole na Mshikamano Majengo hivyo baada ya siku 14 magari yagawenywe kutokana na njia zinazohusika. 

Josephaty Maganga

Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Jeseph Mafulu amesema ofisi yake inahitaji siku 10 ili kuboresha stendi ya Makole ambayo ipo tayari aweze kuongezwa upana ambao unaweza kuchukua idadi kubwa ya magari ya daladala ya njia za upande huo

Tulishatenga maeneo ya Daladala kutokana na jiografia ya jiji la Dodoma zaidi ya miezi 8 sasa kama ile ya makole na mshikamano kule majengo ambapo kutokana na udogo wa stendi hii ya sabasaba ambayo inaukubwa wa heka mbili pekee na kuwa na uwezo wa kuchukua magari ya daladala si chini ya 200 tofauti na sasa ambapo zaidi ya magari 2000 yanabanana pale na kusababisha msongamano mkubwa

Sasa hivi tumeshaanza kumwaga kifusi naomba siku mbili za leo na kasha ili kikishasambazwa paanze kutumika na kuhusu taa na ukarabati mwingine tutaufanya ndani ya siku hizo 10 naomba kuwasilisha.

Jeseph Mafulu

Awali katibu wa madereva wa daladala Samwel Mazengo amesema waliamua kugoma kutokana na kuandika maombi kadhaa kwa mkurugenzi wa jiji bila majibu wakati huo wameendelea kuumiza magari kwenye stendi ya sabasaba kutokana na kutofanyiwa ukarabati huku wakiendelea kulipa ushuru

Amesema moja ya malalamiko yao ni udogo wa stendi ukilinganisha na wingi wa magari 2000 yaliyopo, ukosefu wa taa hali inayosababisha abiria kuibiwa, wenye bajaji kuingilia abiria wao huku wakishusha nauli, msongamano wa wafanyabiashara wadogowadogo wakiwemo wa matunda, mbogamboga, wachoma mishika na chipsi, matoroli na urembo

 

Post a Comment

0 Comments