📌Na Ramadhan Hassan
WAZIRI mpya wa Mawasilino na Teknolojia ya Habari,Dk.Faustine Ndugulile ameanza kazi kwa kukutana na watendaji wa Wizara hiyo huku akiahidi kuhakikisha Wizara hiyo inakuza pato la Taifa pamoja na kujenga uchumi wa Kidijital.
Akizungumza jna wafanyakazi wa Wizara yake,Mtumba Jijini hapa, Dk.Ndugulile amesema sekta hiyo ni lazima iwe na mchango mkubwa katika pato la taifa kama ambayo ameagiza Rais Dk.John Magufuli.
“Sekta hii ya mawasilino lazima iwe na mchango katika pato la Taifa na Rais ametuelekeza katika hilo.Tunawajibu wa kuhakikisha tunaenda kwa kasi ili makusudia yake yaweze kuonekana.Sasa hivi tunataka kujenga uchumi wa Kidijital na hilo limegusiwa katika ilani ya CCM,”amesema.
Amesema sekta ya Mawasilimo na Habari ni mtambuka ambayo itagusa takribani Wizara zote na ni sekta ambayo inagusa maisha ya kila mtanzania hivyo ni lazima watendaji wajitoe kuhakikisha maendeleo yanapatikana.
“Maisha ya sasa yote yapo katika habari sisi tupo kuhakikisha sekta hii inasimama katika maisha ya mtanzania pamoja na kutatua kero mbalimbali.Itakuwa ni sekta mtambuka tutafanya mawasilino na Sekta mbalimbali kuhakikisha huduma za serikali na mawasilino na wananchi tunaziboresha,”
amesema.
Pia,amesema Tanzania imefikia uchumi wa kati hivyo ni lazima Wizara ianze maandalizi ya kuingia katika mifumo ya Kidigital kwa lengo la kuhakikisha maendeleo yanapatikana.
“Tanzania inahamia uchumi wa kati na katika uchumi wa kati kuna jambo linaendelea mapinduzi ya nne ya viwanda ambayo ni mifumo ya Digital itakuwa ni mambo muhimu,sasa tumepewa Wizara mpya ni lazima tuanze maandalizi wakati tunahamia uchumi wa kati,”amesema.
mwisho
0 Comments