📌Na HAMIDA RAMADHANI.
MKUU wa chuo Kikuu cha
Dodoma(UDOM)Balozi Mhandisi John Kijazi ameutaka uongozi wa chuo hicho kuweka
mfumo na utaratibu mzuri wa mawasiliano kati yao,utumishi na wanafunzi pale
kutapotokea changamoto mbalimbali.
"Wanafunzi wengi hulazimika kwenda ngazi za juu na wengine kufanya vurugu kutokana na chuo husika kutokuwa na mfumo mzuri wa mawasiliano kati ya uongozi ,utumishi na wanafunzi hivyo nimeongea na watumishi wa hapa UDOM kuweka utaratibu mzuri wa kuwasilikiza wanafunzi na kama uongozi wa chuo utashindwa ndipo waende juu"amesema Kijazi
"Nguzo kubwa ni kujiamini hata kama umejiajiri usiogope maisha, fanya kazi kwa juhudi na maarifa ,na onyesha kuwa umetoka Udom kwani tukifanya kazi kwa pamoja tutalijenga Taifa letu "
Amesema Balozi Kijazi
Nae Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Gaudensia Kabaka amesema tangu kuanzishwa chuo hicho mwaka 2007 kimekuwa na wahitimu ambao wamechangia kuleta maendeleo katika jamii .
Aidha amesema chuo
kimeweka mikakati na vipaumbele vya maendeleo hususani kuhusisha ukaguzi wa
mahesabu ili kuisaidia Baraza kudhibiti mali za umma na kuhakikisha chuo
kinafuata sheria na taratibu za fedha.
Athumani Makona ni mhitimu wa PHD ya mipango ya kustaafu ambapo amesema atatumia elimu yake kuwasaidia wastaafu kwa kuwashauri na kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kujiandaa kabla ya kustaafu kutokana na wengi wao kuwa na maisha magumu baada ya kustaafu kwa kutokujiandaa mapema.
0 Comments