📌Na DEVOTHA SONGORWA.
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji wa Mzakwe wenye thamani ya zaidi ya milioni 200 unaotarajiwa kupunguza adha ya maji kwa mkoa wa Dodoma.
Pia amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuhakikisha vinachimbwa visima vingine vikubwa viwili kuongeza nguvu ya upatikanaji wa maji.
Waziri Aweso ameyasema hayo usiku wa Disemba 20,2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari alipofanya ziara ya kushtukiza kukagua utekelezaji wa mradi wa maji wa Mzakwe unaofanywa na Kampuni ya Shanxi ambapo amesema Wizara imeipatia Bilioni Moja Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma(DUWASA) kutatua changamoto hiyo.
"Tunafahamu hivi Sasa Jiji la Dodoma kuna watu wengine ndiyo maana kunakuwa na shida ya maji tulikaa kikao na DUWASA disemba 10wakasema Kuna mradi unaendelea usiku na mchana Sasa tukataka kujiridhisha na nikweli tumekuta kazi inafanyika lakini kisima hiki hakitoshi namuagiza Katibu Mkuu kuchimbwe visima vingine viwili haraka tumalize hii shida",alisema Waziri Aweso.
Amesema uhitaji wa maji mkoa wa Dodoma ni lita milioni 103 wakati uzalishaji wa sasa ni lita milioni 66 ikionyesha upungufu wa lita milioni 37 huku akibainisha kuwa kisima hicho kinatarajiwa kuzalisha lita 400,000 kwa saa 24.
"Ina maana tukichimba visima vitatu tutakuwa na Lita milioni 1200,000 kwa saa Ina maana kwa saa 24 tutakuwa na lita million 28 na tumewaagiza mawakala wa uchimbaji visima DCCA wanachimba visima 10 maeneo ya Ihumwa, Zuzu na Chamwino kwa hivyo tunaamini Dodoma itakuwa na maji ya kutosha",ameeleza Waziri huyo.
Pia Waziri Aweso ametoa onyo kwa baadhi ya watu wanaofanya mgao wa maji bila kufuata utaratibu akisema wizara haitomvumilia yeyote anatakayebainika kufanya ubabaishaji kwani serikali imejipanga kufanya kazi usiku na mchana kufikisha kwa kila mtanzania huduma hiyo.
"Tumeshalipa fidia kwa watu wa eneo la Faru kupisha mradi wa maji sisi Wizara tumeanzisha standard Gauge yetu ya miradi mikubwa ya maji tuna raslimali toshelevu tuan Ziwa Tanganyika,Nyasa,Mto Ruvu tumetekeleza mradi mkubwa wa kutoa maji Ziwa Victoria tumepeleka Tabora,Ingunga Nzega ni wakati wetu Sasa kuhakikisha tunayafkisha Singida,Dodoma ili watanzania wapate Huduma ya maji",amesema Waziri huyo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji DUWASA ,Mhandisi, Aron Joseph amesema mradi huo unafanywa na Kampuni ya Shanxi akieleza kuwa kisima kitakuwa na urefu wa mita 150 ambapo hadi sasa kimefikia theluthi ya utekelezaji wake mradi huo ulitarajiwa kukamilika ndani ya siku 60 lakini watatekeleza kwa muda wa siku 30.
"Kisima hiki kina uwezo wa kuzalisha maji mita 400 kwa saa sawa na mita 400,000 kwa siku nia tupate ujazo wa maji mita 21,000 kwa siku kutoka eneo hili na uchimbaji umefikia theluthi tunatakiwa kuchimba mita 150 Sasa anakarbia mita 40 visima vinatoka kwenye miamba unaweza kukuta chumvi au maji baridi na Kuna kiwango Cha chumvi kikichowekwa na TBS kwa ajili ya matumizi ya binadamu kikizidi hatuwezi kuchimba",amebainisha Mhandisi Joseph.
Aidha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi, Anthony Sanga akaahidi kutekeleza maagizo yaliyotolewa huku akiwahimiza watanzania kuendelea kutunza vyanzo vya maji katika maeneo yao.
"Hapa panaitwa Mamba ya mbali tutafanya tukiyooelekezwa na Mheshimiwa Waziri huu ni mtambo mkubwa tumechukua mkondo wenye maji mengi na Ni maji baridi hiki kitakwenda kwa milimita 400 au inchi 16 Hawa ndiyo waliokuwa wanachimba ule mradi mkubwa wa bilioni zaidi ya 500 Arusha na gharama za kisima hiki inarange milioni 200hadi 2500 kwa sababu kina diameter kubwa Sana",ameeleza Mhandisi Sanga.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikagua mradi mkubwa wa maji usiku wa kuamkia leo eneo la Mamba ya mbali, ulipo Mzakwe jijini Dodoma akiambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi, Antony Sanga na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dodoma(DUWASA) Mhandisi Aron Joseph.
Mradi mkubwa wa maji unaofanywa na kampuni ya Shanxi katika eneo la Mamba ya mbali, Mzakwe unaotarajiwa kuzalisha lita 400,000 kwa saa 24 utakaosaidia kuondoa adha ya maji jijini Dodoma.
0 Comments