📌Na Mwandishi wetu .
WAZIRI
wa Maji Mh.Jumaa Aweso amewataka wataalamu wa maji wa Mamlaka za Maji nchini na
Wakala wa Maji Vijijini kutambua kuwa Wizara haijaajiri vibaka bali wataalamu
wenye Taaluma hivyo yawapasa kuisaidia kwa kufanya kazi kwa weledi badala ya kujinufaisha wao wenyewe
Aweso
ametoa agizo hilo jijini Dodoma katika kikao na watendaji wa mamlaka ya
maji safi na usafi wa mazingira jijini Dodoma (DUWASA) ambapo ameonesha kukerwa
kwake kufuatia watendaji wabadhilifu.
“Wizara
ya maji haijaajiri vibaka,Wizara ya maji imeajiri wataalamu wenye Taaluma
ambazo wamezisomea kwenye vyuo mbalimbali,watumie Taaluma yaokuisaidia Wizara
yetu ya Maji,hatuwezi sisi viongozi wa Wizara ya Maji kuona taswira yetu
iharibike kanakwamba hii ni Wizara ya wizi."Waziri Aweso.
Ameiagiza
Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Dodoma (Duwasa) kuondoa kero ya maji
katika jiji la Dodoma na kuongeza kuwa changamoto ya maji imekuwa kilio kwa wakaazi
wa hao kutokana na watu na kuomba mamlaka itafute njia mbadala ya kuondoa kero
hiyo.
“Katibu
Mkuu wewe umefanya kazi Dodoma naomba mtushauri mambo mengine sio lazima afanye
Rais,naomba wekeza nguvu hapa,kwa sababu wimbi kubwa la watu wanakuja
Dodoma”Amesema.
Mbali
na hayo amewapongeza DUWASA kwa kazi wanayoifanya na kuwataka kuongeza nguvu
zaidi katika huduma kwa wateja na kuhakikisha huduma inawafikiawakazi wa jiji
la Dodoma kama inavyostahilikatika maeneo yote.
Naye
katibu mkuu wizara ya maji Mhandisi Anthony Sanga amesema kuwa licha ya Dodoma
kuwa jiji changamoto ya maji imekuwa ni sehemu ya kilio kwa wananchi hivyo
Mamlaka inapashwa kuongeza kasi ya uwajibikaji.huku Naibu katibu mkuu injinia
Nadhifa Kemikimba akisema mamlaka inapaswa kuongeza kasi ili kuondoa kero ya
maji na wananchi wapate maji safi kwa matumizi yao ya kila siku.
0 Comments