📌MWANDISHI WETU.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameanza kazi ya kuwatafuta wamiliki wa ardhi walioshindwa kuchukua hati zao kwenye ofisi za Ardhi za mikoa kwa kuwapigia simu wamiliki wa jiji la Dar es Salaam na kuwataka kuzifuata hati zao katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Desemba 29, 2020.
Mikoa mingine na idadi
ya Hati katika mabano ni Singida (201), Morogoro (1,345), Mtwara (470), Lindi
(235), Ruvuma (118), Kilimanjaro (224), Manyara (143), Arusha (135), Tanga
(711), Mbeya (266), Iringa (137), Njombe (45), Rukwa (23), Songwe (68), Kigoma
(555), Tabora (626), Katavi (261), Mwanza (1,532), Geita (251), Simiyu (213),
Kagera (382), Shinyanga (817) na Mara (559).
Lukuvi amewahimiza
wananchi kujitokeza kuchukua hati kwenye ofisi za ardhi za mikoa na kusisitiza
kuwa, hivi sasa wamiliki wamerahisishiwa uchukuaji hati katika ofisi za ardhi
za mikoa tofauti na huko nyuma ambapo walilazimika kusafiri mpaka ofisi za
kanda zilizohusisha zaidi ya mikoa miwili.
Alisema, mmiliki
yoyote wa ardhi anayejua amelipia kodi pamoja na tozo zote ajue kwamba ni
miongoni mwa watu ambao hati yake imekamilishwa na iko katika ofisi ya Msajili
wa Hati.
"Tafadhali kama
una hati na kiwanja kilichopimwa na umelipa kodi na tozo zote za kutayarishiwa
hati nenda ofisi ya ardhi mkoa umtafute msajili wa hati ili uthibitishe na
uchukue hati, tunataka zoezi hili liishe haraka kila mwenye hati afuate
mwenyewe na kama kuna kodi anadaiwa alipe" alisema Lukuvi.
Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi aliwataka makamishna wote Wasaidizi wa Ardhi katika
mikoa kuhakikisha wanafuatilia katika kila wilaya na kuangalia aliyemilikishwa
kama hajachukua hati akachukue mwenyewe na isiwe zaidi ya siku 30 kuanzia
tarehe 29 Desemba 2020.
Katika hatua nyingine,
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewataka wamiliki
wa ardhi wanaotaka kujenga kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu zote
wakati wa kufanya ujenzi.
Lukuvi alisema, sheria
inamtaka mmiliki wa ardhi anayetaka kufanya ujenzi kupata kibali kutoka
halmashauri za miji, manispaa na majiji na kuongeza kuwa sheria hiyo inakataza
kufanya ujenzi bila kibali kutoka mamlaka husika.
" Naelekeza
watendaji wote wawe wa ardhi au mipango miji kuhakikisha sheria zinafuatwa kwa
kudhibiti ujenzi holela na sheria inakataza kabisa kujenga bila kupata kibali
kutoka katika mamlaka husika" alisema Lukuvi.
Kwa mujibu wa Lukuvi,
zoezi la urasimishaji linaloendelea sasa maeneo mbalimbali ni kwa majengo
yaliyojengwa tu na kusisitiza kuwa zoezi la urasimishaji isiwe sehemu endelevu
ya kuvunja sheria na kubainisha kuwa angetaka kuona maeneo yote ya miji hasa
Dodoma yanajengwa kwa kupatiwa kibali.
Aliwataka wataalamu
wote hasa waliopo halmashauri katika yale maeneo yaliyotangazwa
kimji kwa mujibu wa sheria wananchi wake waelimishwe kujenga katika
viwanja vilivyopangwa na kupimwa na wawe wamepatiwa vibali na mamlaka za
halmashauri husika.
" hatua
zichukuliwe kuzuia jambo hili tunataka miji endelevu ambayo wananchi wanaishi
na kujenga kwa mujibu wa sheria" alisema Lukuvi
0 Comments