Maganga,ameyasema hayo wakati akizungumza na
wazazi pamoja na viongozi mbalimbali katika sekta ya elimu kwenye Mahafali ya
kwanza ya shule ya awali na msingi ya Ellen White, iliyopo Nzuguni jijini
Dodoma.
Amesema,kutokana na serikali kuhamia Dodoma hivi
sasa mahitaji ya shule yameongezeka kutokana na idadi kubwa ya watu walipo.
“Tunawakaribisha sana wawekezaji maeneo bado
yapo mengi kwa ajili ya kufanya uwekezaji hivyo niwaombe waje kwa wingi ili wawekeze
katika sekta ya elimu”amesema Mganga
Aidha, amesema katika jitihada za kukuza elimu
katika Wilaya ya Dodoma mikakati iliyopo ni kujenga madarasa, nyumba za walimu
mabweni pamoja na kuboresha miundombinu mingine ya elimu.
“Pamoja na jitihada hizo lakini niwatake
walimu, waratibu elimu kata pamoja na maafisa elimu kila mmoja atimize wajibu
wake ili kuhakikisha kuwa jiji la Dodoma elimu inakuwa”amesema Maganga
Mwenyeki wa Kamati ya shule hiyo Mchungaji
David Mbaga, amesema kuwa lengo la shule hiyo ni kuhakikisha kuwa inatoa elimu
bora ambayo itawawezesha wahitimu kuwa na uwezo wa kujitegemea.
Mkurugenzi wa shule hiyo Simon Ikwabe, amesema kuwa malengo ya shule hiyo ni kuwa ya mfano nchini katika utoaji wa elimu bora inayowawezesha wahitimu kuweza kujitegemea.
0 Comments