WASHIRIKI DODOMA KATI WATOA YA MOYONI KATIKA SABATO YA MWISHO 2020:



📌 
FAUSTINE GALAFONI.

Kama  ilivyoada kwa makanisa mengine  ya Kiadvetista,Siku ya Jumamosi ya Tarehe 26,2020 ilikuwa ni Sabato ya mwisho  ya mwaka 2020  hivyo hivyo kanisa la Waadventista Wasabato Dodoma kati  liliungana na makanisa mengine Duniani katika ibaada ya Mwisho ya mwaka 2020 .

 Wakizungumza katika mahojiano maalum na mtandao huu  katika Sabato ya Mwisho ya Mwaka  2020 iliyofanyika katika Kanisa la Waadventista Wasabato Dodoma kati,baadhi ya Washiriki wa kanisa  hilo walisema kuwa ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kuwezesha kufikia Sabato ya Mwisho kwa mwaka 2020 .

 Emiry Jackson,Neema Maige,Mark Imori,Emmanuel John Mkolwa,Zena Thadeo,ni miongoni mwa washiriki wa kanisa la Waadventista Wasabato Dodoma kati   waliopata fursa ya kuzungumza na mtandao huu huku wakielezea ukuu wa Mwenyezi Mungu kwa kuwasafirisha Salama hadi Mwishoni mwa Mwaka 2020 na kuwa na matarajio makubwa ya kuupokea mwaka 2021.

 “Ni jambo la pekee kumshukuru Mungu mpaka tunafikia Sabato ya Mwisho ya Mwaka 2020 tumevuka milima na mabonde sasa tegemeo letu kubwa ni kuendelea kumtumainia Mungu kwa Mwaka Mpya 2021 hakika atatuvusha Salama na unapomtegemea Mungu yote yanawezekana”alisema Emiry Jackson.

 Mmoja  washiriki  Mwingine aliyepata Fursa ya kuzungumza na mtandao huu  ni Mark Imori ambapo alibainisha kuwa ni jambo la Kushukuru Mungu kwa Kutuongoza.

“Kubwa zaidi tunamshukuru Mungu kwa kutuongoza ametupigania mpaka hapa tulipo na jambo kubwa ni kuanzishwa kwa ujenzi wa Kanisa jipya la Waadventista Wasabato Kisasa na hali ikiendelea vizuri”alisema Imori.

Emmanuel John Mkolwa  ni Afisa Usafirishaji kanisa la Waadventista Wasabato jimbo la kati mwa Tanzania [CTF]ambapo naye alipata fursa ya kuzungumza na mtandao huu  na kubainisha kuwa ni jambo la furaha kwa kuumaliza mwaka 2020  na kusema kuwa jambo kubwa ni kuyakabili Mambo kwa imani.

 Kama unavyojua  kazi zetu ni kutembelea maeneo mapya kila siku hasa tunapokuwa katika majukumu mazito ya kuwasafirisha viongozi wetu kwa ajili ya kazi za utume tunakumbana na vikwazo ,mbalimbali njiani ,hususan unapokutana na madereva ambao hawazingatii kanuni na utaratibu za  usalama barabarani kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tunakabiliana nayo kwa kuwakwepa na kuepusha kusababisha ajali na kuwafikisha viongozi salama kabisa jambo ambalo ninaondoka nalo mpaka mwaka 2021 ni kuyakabili mambo kwa iman 
amesema.

 Pia , John alitumia fursa hiyo kuvipongeza vyombo  vya Habari vya Kanisa la Waadventista Wasabato chini ya Mkurugenzi wake Mchungaji Christopha Ungani kwa kuendelea kujiimarisha zaidi katika  kueneza Ukweli wa Biblia kwa Mataifa Mbalimbali.

Wakati huohuo,Wakristo waliaswa kumshirikisha Mungu pekee pindi wanapofanya jambo ili kuepusha vizuizi vinavyoweza sababishwa na walimwengu.

Wito huo ulitolewa  Disemba 26,2020 jijini Dodoma na Mzee wa kanisa
la Waadventista Wasabato Dodoma kati  Mwinjilisti Emmanuel Mapande
katika  ibaada kuu ya Sabato kanisani hapo ambapo ilikuwa Sabato ya
Mwisho kwa mwaka 2020 ambapo alisema  kuwa mwanadamu anapokuwa na jamno kubwa ni kheri kusema na BWANA kwani  katika kumshirikisha mwanadamu anaweza kuleta vizuizi kwa kukatisha tamaa.

 “Ukiwa wewe una jambo lako Fulani unataka kulifanya nataka nikuambie sema na BWANA wako  pekee ili kuepusha vizuizi ambavyo vinaweza kujitokeza “alisema.

Hivyo,Mwinjilisti Mapande alibainisha kuwa tumaini lililopo kwa
Wakristo licha ya changamoto zilizopo ni Yesu Kristo kwani  ni tumaini
 hilohilo ambalo  walikuwa nalo wakoma pindi walipokuwa wakihitaji
Chakula na waliweza kuvuka salama katika kukabiliana na changamoto
hizo..

 Tunatembea katika shida na changamoto mbalimbali lakini tumaini kuu ni Yesu Kristo”amesema.

 

Post a Comment

0 Comments