WALIMU WANAFUNZI WA UDOM (UDOSTA) WASAMBAZA UPENDO 'JENERO'

 



📌MWANDISHI WETU

WAHENGA walinena  kutoa ni moyo,na moyo wanoauonesha wanafunzi  kutoka chuo kikuu cha Dodoma ndani ya Umoja wa Walimu wanafunzi (-University of Dodoma Student Teacher’s Association) UDOSTA)  ni moyo wa upendo,ukarimu na kujali jamii  inayowazunguka.

Leo walimu wanafunzi wa UDOSTA wametembelea hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma kugawa mahitaji mbalimbali.

Mwenyekiti wa Umoja hu Teddy Gilosa amesema wameamua kutembelea hospitalini hapo na kugawa vitu mbalimbali kwenye wodi za watoto baada ya kuguswa kufanywa.

Wapo watu wengi wamelazwa kwenye hospitali zetu na hawana wa kuwapa faraja,hivyo UDOSTA tumeamua kuwa wafariji kwa kundi hilo ili nao wajione ni sehemu ya jamii yetu na sio kujiona kama wametengwa.

Teddy Gilosa

UDOSTA ambayo inadhaminiwa na Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kimetoa msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwemo sabuni,dawa za meno,mafuta pamoja na pampasi kwa ajili ya watoto na mama zao waliolazwa katika hospitali hiyo.

Katibu wa UDOSTA Alexander Mwangoka amewashukuru wadau wote walioshirikiana katika kufanikisha zoezi hilo.










Sanjari na kutoa mahitaji mbalimbali,Walimu hawa tarajali pamoja na walimu waliopo masomoni walihakikisha wanaiacha hospitali hii ambayo ni tegemeo la mkoa wa Dodoma ikiwa katika hali ya usafi.











Post a Comment

0 Comments