📌Na Barnabas kisengi
Mkuu wa wilaya ya
Mpwapwa Jabir Shekimweri amewataka wakina mama wajawazito wilayani mpwapwa
kutumia vituo vya afya vilivyojengwa na serikali kwenda kujifungulia huko
badala ya kukimbilia katika hospital ya wilaya na kusababisha msongamano usio
na umuhimu katika hospital hiyo.
Shekimweri ametoa
kauli hiyo katika kuadhimisha sikukuu ya uhuru leo December 09 wakati
kuzungumza na wakinamama wajawazito wapatao 55 ambao wapo katika hospital hiyo
wakisubiri kujifungua na kuacha kutumia vituo vya afya vya maeneo ambayo
wanaishi.
"Mama zangu na
dada zangu sasa imefika wakati mnatakiwa kunitumia vituo vya afya vya Kata kwa
sababu vinatoa huduma zote Kama zilizopo hapa wilayani kwa kuwa serikali ya
awamu ya tano imejenga Vitui hivyo na kuwaletea wataalamu wakiwemo madaktari na
waunguzi sawa na waliopo "amesema shekimweri
Shekimweri akaelezea
kuwa serikali imetumia zaidi ya shilingi billion mbili kujenga vituo vya
afya Vinne vilivyo kamilika na vinatoa huduma sasa ifike wakati wakinamama
mvitumie vituo kwa kupatiwa huduma bora na yakisasa.
Kwa upande wake
kamanda takukuru wilaya ya mpwapwa Juliet Mtui amewataka wakina mama wajawazito
kuepukana na kutoa rushwa pindi wanapokuwa katika hospital,vituo vya afya na
zahanati wanako patiwa huduma kwani kupewa huduma ni haki yao ya msingi hivyo
wajiepushe kabisa na kuichukia rushwa na pindi watakapo ombwa rushwa au kuona
kunaviashiria vya rushwa wawe wepesi kutoa taarifa.
"Wanawake
wenzangu leo ukiwa ni siku ya kumbukizi ya sikukuu ya uhuru pia ni siku ya
dunia kupiga Vita rushwa hivyo muwe makini na vitendo vya rushwa ya ngono, pia
mnapokuwa mnapatiwa huduma usikubali kuombwa chochote na mtoa huduma kwani ni
wajibu wake kukupatia huduma unapo kuwepo maeneo haya". Amesema mtui
Katika maadhimisho ya
sherehe za uhuru ofisini ya mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi
na usalama na wadau mbalimbali wakiwemo watumishi wa ofisi ya mkuu wa wilaya na
kikosi cha JKT na kiongozi wa chama cha mapinduzi CCM wilayani hapo
wamefanya usafi katika eneo la hospital na kuchangia kutoa damu ambapo wameweza
kutoa jumla ya unit 27 za damu na kukabidhi hospital hapo
Mwisho
0 Comments