WAFUGAJI TUMIENI KITUO CHA MIFUGO KUJIFUNZA,UFUGAJI BORA.

 


📌BARNABA KISENGI:

Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Jabir Shekimweri amewataka wafugaji wilayani humo kutumia kituo cha Mifugo Tariri kujifunza ufugaji bora na wenye tija ili kuweza kuwa na mifugo michache yenye tija na kubadilisha uchumi.

Ametoa kauli hiyo mara baada ya kuwatembelea baadhi ya wafugaji wa Kata ya luhundwa na kugundua,bado wanafuga kizamani kwa kuwa na mifugo mingi isiyokuwa na tija na badala ya kunitumia kituo cha utafiti wa mifugo tariri mpwapwa kujipatia elimu ya ufugaji bora na wakisasa. 

 "kwakweli inasikitisha kuona kituo cha tariri kinawafaidisha wafugaji kutoka nje ya mpwapwa wanapata elimu ya ufugaji bora huku wafugaji wazawa wa mpwapwa hawatumii fursi hii ya uwepo wa kituo hichi ambacho kina wataalamu wa kutosha na wanatoa elimu bure kwa wafugaji sasa wafugaji wa baadhi ya maeneo ya mpwapwa bado wanafuga kienyeji inasikitisha sana" amesema shekimweri 

 " unakuta zizi lina ng'ombe 400 ambao wamekonda na hawana ubora wakati angeweza kuwa na ng'ombe 100 wenye uzito mkubwa ukiangalia mifugo iliyopo hapa tariri inavutia kwa ukubwa na uzito sasa mifugo Kama ya tariri nataka kuiona kwa wananchi huko vijijini itawabadilisha kimaisha na kiuchumi hapa mpwapwa "amesema shekimweri

 Mwisho

 

Post a Comment

0 Comments