📌Na DEVOTHA
SONGORWA.
WAANDISHI wa habari
jijini Dodoma wamepatiwa mafunzo ya uandishi wa habari za kisayansi kuwajengea
uwezo wa kufikisha taarifa sahihi kwa jamii wakiwemo wakulima na wafugaji.
Mafunzo hayo
yaliyoanza Jana yakitarajiwa kuhitimishwa leo yanahusisha mikoa ya Singida na
Dodoma yanatolewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na teknolojia Nchini (COSTECH)
kama sehemu ya kuwapa ujuzi mpya waandishi wa habari na watangazaji kuondokana
na uandishi wa mazoea.
Akizungumza katika
semina hiyo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (COSTECH) DK. Philbert Luhunga amesema
lengo la mafunzo hayo kwa waandishi wa habari ni kuwajengea uwezo wa
kuandika taarifa hizo za kisayansi kwa lugha rahisi ili wananchi waweze kuelewa
na kupata matokeo yaliyokusudiwa na yatafanyika mikoa yote nchini.
“Lengo ni taarifa za
kisayansi zitumiwe na wengi na serikali katika kufanya maamuzi yake inauma sana
unafanya utafiti halafu kwa lengo la kubadili sera halafu hauendi huko kwa sababu
kuna gape kwa sababu ya vyombo vya habari Tanzania wanataka kuona mchango wa
wazi wa Sayansi na teknolojia lazima kuwe na flow of information kutoka kwa
watafiti hadi kwa walaji”,alisema Luhunga.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Kituo cha utafiti nchini (TARI-MAKUTUPORA ) Cornel Massawe
ameishauri COSTECH kuunda Jukwaa la Wabunifu,watafiti na waandishi wa
habari ili teknolojia zinazopatikana kupitia utafiti ziwafikie
walengwa kwa urahisi na kuleta tija .
“Kuna wakati baadhi ya
watafiti wanakosa lugha nzuri au nyenzo za kuwafikia walengwa wa hizo
teknolojia ni wakati sasa wa COSTECH kutengeza jukwaa ili tufanye kazi kwa
pamoja hapa waandishi wa habari watakuwa kati yetu wana sehemu kubwa sana
katika hili”,ameshauri Masawe.
Nao baadhi ya Waandishi
wa Habari waliohudhuria mafunzo hayo wameishukuru COSTECH kuwapa mafunzo
hayo yatakayosaidia kutekeleza majukumu yao katika hali ya ubora na kukidhi
mahitaji ya jamii.
Saida Issa ambaye ni
mwandishi wa habari wa gazeti la Zanzibar leo amesema “mafunzo hayo yamemjenga katika
kazi yake hasa kufanya utafiti na kujua umuhimu wa taarifa za utafiti ambapo lazima uwe na
takwimu sahihi kutoka kwa wahusika ili usipotoshe jamii.
Aidha Mwandishi wa
habari nwa Mwangaza Fm Nazael Mkude ameeleza kwamba waandishi wengi wamekua
wakiandika kwa mazoea akisema ifike wakati sasa wa vyombo vya habari kuipa
umuhimu nyanja ya kisayansi kwani imechangia pakubwa kukuza sekta ya habari.
“Tumezoea kuandika habari za
michezo,siasa,burudani na zingine sasa naamini tutabadilisha mfumo tujikite
habari za wabunifu tuhakikishe mtu akifungua mitandao asikose habari ya masuala
ya sayansi kama inavyokuwa katika habari zingine nimefurahi sana kwa mafunzo
haya”alieleza Mwandishi huyo wa habari.
0 Comments