📌FAUSTINE GIMU GALAFONI.
Mkurugenzi Idara ya Elimu kanisa la
Waadventista Wasabato jimbo kuu la
Kusini mwa Tanzania Bi.Devotha Shimbe amewaasa waumini wa Kanisa la
Waadventista Wasabato hapa nchini kuchangamkia fursa ya Kuwekeza elimu
kwa kujenga shule katika makao makuu ya nchi Dodoma ili kuwajengea zaidi
maadili ya kiroho na yampendezayo Mungu Watoto wa shule za Kiadventista.
Bi.Shimbe amebainisha hayo jijini Dodoma
wakati akifanya mahojiano Maalum ambapo amesema
kanisa linatambua mchango mkubwa unaofanywa na mshiriki mmoja mmoja hivyo ni
muhimu washiriki wakawekeza katika suala la elimu hali itakayosaidia
kuwaandaa watoto kuwa na maaadili mema kwani elimu ya maadili ya kiadventista
ni moja ya uinjilisti.
Hivyo,Bi.Shimbe amebainisha kuwa elimu inayopatikana
katika taasisi za elimu za kanisa la Waadventista Wasabato zimejengwa
zaidi katika maadili na falsafa ya msingi wa Biblia ambapo watoto huandaliwa
katika maisha ya sasa na maisha ya milele.
Aidha, Mkurugenzi huyo wa Idara ya Elimu kanisa la
Waadventista Wasabato jimbo kuu la Kusini mwa Tanzania amebainisha kuwa
Union ina mpango wa kujenga Chuo kikuu katika makao makuu ya nchi Dodoma
ambapo Jumla ya ekari 350 zilishapatikana kwa ajili ya ujenzi huo
0 Comments