📌DEVOTHA SONGORWA.
VIJANA nchini wametakiwa kusimamia
malengo yao kwa kutumia vyema nguvu walizo nazo kwa mustakabli wa Taifa kwa
ujumla badala ya kuogopa changamoto.
Hayo yamesemwa na Katibu
Mkuu wa Umoja wa Vijana Taifa kupitia Chama Cha Mapinduizi
(UVCCM),Raymond Mwangwala wakati akizungumza na gazeti hili ofisini kwake
kuhusu namna watakavyomuenzi aliyewahi kuwa Kaimu Katibu wa Idara ya
Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM,Egla Mamoto aliyefariki dunia Disemba 27 mwaka
huu.
Alisema vijana wengi wamekuwa
wamekuwa wakikata tamaa katika safari yao ya kusaka mafanikio akiwataka kutumia
mwaka 2021 kuwa na mabadiliko kwa kusimama imara na kutokukubali kushindwa wala
kuyumba kuhakikisha wanakuwa na mchango kwa nchi.
"Cha kumuenzi ni katika
maandiko aliyoyaacha na kama umoja wa vijana ni kuenzi mambo ya Egla
utu,upambanaji vijana wengi wakishindwa kidogo tu wanarudi nyuma anaanza
kutukana kumbe inatakiwa utulie, simama jipukute vumbi endelea na safari no
retreat no salenderna kusimama katika yale wanayoamini yana mchango kwa
Taifa",alisema Katibu Mkuu huyo.
Akizungumzia mchango wake katika
Chama alisema amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinapata
ushindi katika uchaguzi wowote ule na kusimamia katika yale aliyoyaamini
kwa kutumia vipaji alivyojaaliwa wakati wote wa uhai wake akisema
wamepata funzo kubwa.
“Kabla ya umauti kumfika mpaka saa
nne usiku alikuwa akichat katika makundi ya whatsAspp akiwatakia watu kheri ya
mwaka mpya tumejifunza tuwe tayari wakati wote, tunaweza kuwa na mipango yetu
lakini Mungu naye ana mipango yake kwahiyo tuwe na upendo na ushirikiano
tujijenge kwa watu social capital ni kubwa kuliko kujidai na kujiona wewe ni
zaidi yaw engine",alieleza Mwangwala.
Kuhusu mchango wake katika nafasi ya
uongozi kama mwanamke aliwataka wanawake kuiga mfano huo kwa kuonyesha
utuhubutu kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi akisema hakuna
maendeleo katika Tiafa lolote yasiyomtaja mwananmke.
“Kama mwanamke alionyesha kwamba
wanamke anaweza bila kuwezeshwa aligombea nafazi zinazohusu wanaume
alishinda, alifanya kazi zinazohusu wananume alifanya vizuri aligombea nafasi
za wanawake aliperform vizuri alionyesha wanawake tusibaki nyuma tusisubiri
kubebwa tusimame maana wanawake wakisamam watasaidia nchi yao",
alisisitiza Katibu Mkuu.
Aidha alihitimisha kwa kuwataka
wanaume kutambua uwezo wa wanawake na kuwatia moyo pindi wanapoonyesha nia
ya kufanya jambo fulani la kimaendeleo na kuondokana na mtazamo hasi
kuhusu kundi hilo huku akiwataka wazazi kukuza vipaji vya watoto wao kwa kike
na siyo kuwakatisha tamaa.
“Zamani wanawake wakisiasa
walichukuliwa wahuni siyo kweli niwaambie huku katika siasa kuna
maendeleo mwanamke akisimama unajua ni kweli mwanaume anaweza leo kuegemea
mashariki kesho yuko magharibi tuwaamini wanawake wamepewa uwezo mkubwa na
wazazi tuunge mkono vipaji vya watoto wetu",alieleza Mwangwala.
0 Comments