📌NA HAMIDA RAMADHANI.
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake (UWT) Taifa Gaudensia Kabaka amesema kuwa kazi yake kubwa ni kuhakikisha
anaongeza uchumi ndani wa UWT kuweza kujitegemea na kuacha kuombaomba katika
chaguzi zote kuanzia chini Matawi, Kata, Wilaya, Mkoa hadi Taifa.
Ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati
alipokuwa akizindua shule ya awali ( Chekechea) ya Umoja wa Wanawake Tanzania
UWT ambapo amesema ni lazima umoja huo uwe na vitega uchumi.
" Sasa mkoa ndio huu umeniita
nije kuzindua vitega uchumi vyetu siwezi kuzingua zingua kusema nimechoka
Lazima nije kufanya jambo hili,"amesema Kabaka.
Kabaka Amesema hakuna anayebisha
uchaguzi Mkuu 2020 kundi la akinamama walijitoa kuhakisha Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kinapata ushindi wa kishindo.
"Nimepita Mikoa mingi hapa
Tanzania na nimeshuhudia wanawake walivyokuwa wakijitoa kwenye mikutano ya
hadhara na hata mikutano ya ndani na hata ya kitaifa waliokuwa wakiudhuria kwa
wingi ni wanawake. amesema Kabaka.
Amesema siasa ni uchumi kwani hata
katika kipindi cha Uchaguzi zinahitajika fedha kwaajili ya kuendesha uchaguzi
hivyo ni lazima kuwe na vitega uchumi na sio kuwa ombaomba.
“Leo tumezindua miradi miwili
mikubwa jengo kubwa la shule ya awali na Fremu za biashara”Amesema…..na
kuongeza elimu ndio Kila kitu katika maisha na haina kukwepa kwepa Lazima Watu
wataitafuta tu kwa hatua hii tuko sahihi miradi hii inawateja na wadau elimu na
Haya maduka.
"Hakikisheni mnakuwa karibu na
Ofisi za elimu ili kupata maelekezo juu ya uendeshaji na kupata Aina ya walimu
wazuri" .amesema Kabaka
"Kuna wadhibiti ubora ili
wasije kuifungia shule yetu kwa kukosea masharti inawezekana mmefanya mengi
ila kuweza kufanikiwa Lazima tuwe karibu na hao wadhibiti ubora"
Naye Kaimu Katibu UWT Mkoa wa Dodoma
Secilia Ndalu amesema ni jambo la kihistoria kwa
wanawake wa Mkoa na hasa katika hatua hiyo kubwa walioifikia.
Amesema walianza ujenzi mwezi Agosti
2018 hadi Desemba 2019 kwa kusafisha eneo kwaajili ya ujenzi kwa kuwachangisha
wadau wetu mbalimbali wakiwemo madiwani wa viti maalumu wabunge mwenyekiti uwt
na wana CCM mbalimbali .
"Ujenzi wa maduka ulianza Mwezi
Desemba 2019 hadi Desemba 2020 kwa kupata muwekezaji Ismaili Chande aliejenga
maduka yaliopo mbele ya shule hii na ujenzi huo ulighalimu Milioni 51".
amesema
Mwisho.
0 Comments