📌Na DEVOTHA SONGORWA.
WAZIRI wa Katiba na Sheria Mh. Mwigulu Nchemba ameitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kutetea na kusimamia haki za wanawake na watoto ili kukabili vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Waziri Nchemba ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea ofisi za Tume hiyo kuzungumza na watumishi ambapo amesema wanawake na watoto wamekuwa wakinyanyasika katika maeneo mbalimbali hivyo ipo haja ya kulinda kundi hilo.
"Serikali haiwezi kuendelea kufumbia macho vitendo vya ukatili vinavyondelea na vingi vimekuwa vikifanywa na watu wa Karibu Sana kundi hili lazima lilindwe Tume ishirikiane na wasaidizi wengine wa kisheria tukomeshe vitendo hivi", amesema Wazir Nchemba.
Aidha,amekemea tabia ya baadhi ya watendaji kutumia madaraka yao vibaya kwa kunyima wanawake haki zao na kuwa atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria.
Waziri Nchemba amesema utawala bora isitumike kwa ajili ya maslahi ya watu binafsi,ambapo sambamba na hilo ameipongeza tume ya haki za binadamu kwa kuendelea kuwa na mwelekeo mzuri Katika utendaji wa haki.
Naye,Naibu Waziri wa Katiba na sheria Jofrey Mizengo Pinda amesema serikali itahakikisha inaimarisha taasisi hiyo ya haki za binadamu na utawala bora kwa lengo la kuwasaidia wananchi.
Amehimiza kuwa tume lazima kuwa karibu na wizara inapotekeleza majukumu kabla ya kuyapeleka popote .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora Mathew Mwaimu amesema tume hiyo imekuwa ikiendelea kutoa ushirikiano wa kutetea haki hususani zinazogusa moja kwa moja Katika jamii huku akiipongeza wizara kwa kuendelea kutoa ushirikiano.
"Tutaendelea
kushirikiana na taasisi zingine za Sheria maana peke yetu hatuwezi lazima
tuweke nguvu ya pamoja kufanikiwa hili watoto ndiyo Taifa la leo
tukiwaacha wateseke siyo sawa na wanawake Ni nguzo ya jamii tupo tayari
kutumika kwa ajili yao",alisema Mwenyekiti huyo.
0 Comments